Tanzania kutengeneza ndege aina ya helikopta

Ndege aina ya helikopta
Raia nchini Tanzania wameamkia habari za kushangaza kwamba taifa hilo linaunda ndege.
Gazeti la Tanzania la Daily News limeripoti kwamba ndege hiyo aina ya helikopta inakaribia kukamilika na kwamba habari hiyo imekuwa ikisambaa barani Afrika kwa kasi.
Gazeti la Zambia, Observer linasema kuwa lengo la ndege hiyo itayokuwa ikibeba watu kwa bei rahisi itakabiliana na matatizo ya uchukuzi nchini humo.
Huku gazeti la Cameron, Concord likisema kuwa mradi huo ni wa kihistoria linaongezea kuwa lengo lake ni kutengeza ndege 20 kwa mwaka.
Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu wawili inakaribia kukamilika katika chuo cha ufundi cha Teknolojia cha Arusha na itaanza kufanyiwa majaribio ya kuruka angani baada ya kuruhusiwa na mamlaka ya uchukuzi wa angani nchini Tanzania kulingana na Daily News.

Uingereza yaamua kujiondoa kwenye EU

Asilimia kubwa ya raia wa Uingereza wamepiga kura ya maoni wakiitaka ijiondoe kwenye muungano wa bara Ulaya EU.
Huku asilimia kubwa ya kura zikiwa zimekwisha hesabiwa, asilimia 52% ya raia wa Uingereza wamepiga kura ya kumaliza uanachama wa Uingereza ndani ya EU uliodumu miaka 43.
Watu wanaoishi katika mji London na Scotland ndio waliopiga kura kwa wingi kusalia ndani ya muungano huo.
Wandani wa maswala ya afisi ya waziri mkuu bwana David Cameron,wanasema kuwa sasa Britain imeingia katika eneo jipya.
Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanahofu athari za kujiondoa kwa Uingereza kwenye muungano huo utabainika katika masoko ya hisa huku kukitarajiwa athari kubwa kiuchumi kisiasa ndani na nje ya bara Ulaya
Sarafu ya Euro imepanda katika masoko ya fedha huku Paundi ya Uingereza ikiendelea kuporomoka ikiwa ni ishara kuwa wafanyabiashara wanatarajia Uingereza kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya.
Kwa mujibu wa ripoti waliojitokeza kupiga kura hiyo ya maoni inaonyesha kuwa wengi.
Hadi sasa ni majimbo machache ndio hayametangaza matokeo yao na inaonyesha mchuano ni mkali kati ya wanaotaka kubakia na wale wanaotaka Uingereza kujiondoa ndani ya Umoja huo wa Ulaya.