Takriban watu 38 wameuawa katika mapigano mapya yaliyozuka eneo la Tana River siku tatu tu baada ya watu 12 wa kabila la Pokomo kuuawa katika mashambulizi yaliyofanya na jamii hasimu ya Orma.
Msemaji wa polisi Eric Kirathe amethibitisha kuwa polisi 8 ni miongoni mwa waliouawa katika makabilianao hayo yaliyotokea asubuhi ya leo kusini mashariki mwa Kenya.
Muuguzi akimhudumia mwathiriwa wa ghasia Tana River
Kulingana na shirika la misaada la Red Cross, nyumba zimeteketezwa moto baada ya kijiji hicho kuvamiwa na zaidi ya watu mia tatu.
Tukio hili linajiri siku kadhaa baada ya mashambulizi mengine kutokea kwenye eneo hilo la Tana Delta na kusababisha vifo vya karibu watu kumi na saba.
Jamii za wafugaji wa kuhama hama na wakulima zimekuwa zikizozania rasilmali kwenye eneo hilo la Tana Delta lililo na rutuba nyingi na maji.
Polisi kwa usihirikiano na shirika la msalaba mwekundu wameweza kuokoa manusura. Inaarifiwa watu wameanza kuhama eneo hilo la Tana River kukimbilia usalama wao.
Ramani ya Kenya
No comments:
Post a Comment