Mh.Freeman Mbowe,Mwenyeketi wa CHADEMA Taifa
Dr.Wilbrod Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA
Viongozi wa CHADEMA Taifa
Baadhi ya waandishi
Mkutano na waandishi habari unaendelea.mh.Mbowe anaongea.
1.KIKAO cha kamati kuu kilikuwa cha kawaida ,hakuna jambo la dharula
2.Mchakato wa katiba mpya usiathiri mabadiliko ya sheria nyingine kama mabadiliko ya sheria ya uchaguzi
3.Mwaka 2013,ni mwaka wa nguvu ya
umma,hakuna kubembelazana na serikali.rais kikwete hajajibu madai ya
CHADEMA kwa hiyo atashinikizwa.
4.sehemu ambazo CCM wanaogopa kuitisha uchaguzi,wanalazimishwa kuitisha uchaguzi.kata za arusha mjini,sengerema,nk.ziko 15
5.Uongozi wa KARATU wa CHADEMA
umesimamishwa kwa muda mpaka chama kitakapokamilisha uchunguzi wake
huko.wanasheria Marando na Prof Safari watachunguza kashfa za mtu
mmojammoja huko karatu.,kumekuwa na kashfa kwenye miradi ya maji na
ardhi.
6.Hatua za kisheria kufuatia matukio ya
uchaguzi wa ilemela mwanza,baada ya madiwani 2 kufukuzwa uanachama
ziendelee kuchukuliwa,pia hatua za kisiasa zianzishwe kudai uwajibikaji
wa halmashauri wa jiji la mwanza ili haki itendeke.
7.kamati kuu imetambua kutapatapa kwa
CCM juu ya sera zake za katiba mpya,elimu bure na bei ndogo za vifaa vya
ujenzi.CCM haiaminiki,kwa hiyo CHADEMA iendelee kuunganisha umma ili
CCM iondolewe 2014 na 2015
8 M4C iendelee kwa kasi mapema mwaka 2013,sekretariati itangaze ratiba januari.
9.juu ya hoja binafsi za wabunge wa
CHADEMA zito na mdee(kuhusu uporaji wa ardhi na mabilioni ya
Uswis),pamoja na hoja ya Tundu Lisu juu ya uteuzi holela wa rais wa
majaji,kamati kuu imependekeza maazimio ya bunge yafuatwe na baadaye
kidogo kama hairidhiki kamati kuu itaelekeza nini kifanyike kwa hatua za
ziada
10.Kamati kuu imesikitika kuwa rais
amepuuza barua ya CHADEMA juu ya kuunda tume ya kimahakama kuhusu
mauwaji mbalimbali nchini.hivyo M4C itatumika mwaka 2013 kumshinikiza
rais kujibu barua hiyo na kutekeleza yale barua inaelekeza yafanyike
Kamati kuu imesisitiza kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma,na hakuna tena kubembelezana na serikali.
Taarifa kamili itawajia
No comments:
Post a Comment