MBUYU TWITE AANZA MAZOEZI RASMI YANGA - HUKU SIMBA WAKIMUWEKEA PINGAMIZI TFF





PICHA ZOTE NA GLOBAL PUBLISHER

SALUM KINJE NA PASCAL OCHIENG WA SIMBA ITC ZA KUPATIKANA HIVI KARIBUNI YASEMA TFF - HUKU AYOUB WA MTIBWA AKIIPATA YA KWAKE

Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) limetuma Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Ayoub Hassan Isiko aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea timu ya Bull FC ya nchini humo.

 

ITC hiyo ilitumwa jana (Agosti 30 mwaka huu), hivyo kufanya wachezaji ambao ITC hazijapatikana hadi sasa kubaki wawili tu. Dirisha la usajili wa wachezaji litafungwa rasmi Septemba 4 mwaka huu.

 

Wachezaji ambao ITC zao bado hazijapatikana ni Salum Kinje na Pascal Ochieng kutoka AFC Leopards ya Kenya waliojiunga na Simba. ITC hizo zinatarajiwa kupatikana wakati wowote kwani tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeshaziomba kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) baada ya nyaraka zote zilizokuwa zikitakiwa kupatikana.

USAIN BOLT ATISHA TENA DUNIA

Yohan Blake na Usain Bolt wameng'ara tena kwenye mbio za Diamond League mjini Zurich.

Wajamaica Blake, aliyeshinda medali mbili za Fedha kwenye Olimpiki London, wakimgaragaza Mmarekani Tyson Gay - wamefanya mambo tena.

Stroll: Usain Bolt cruises to victory in the 200m in Zurich 

Usain Bolt akikimbia kushinda mbio za mita 200 Zurich Kinara tena: Usain Bolt akishangilia ushindi wa mbio za mita 200 kwenye mbio za Diamond League mjini Zurich

Winner again: Usain Bolt celebrates after winning the men's 200m at the Diamond League in Zurich

 

SIMBA, YANGA OKTOBA 3 LIGI KUU

Abdallah Juma wa Simba SC, mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kucheza Ligi Kuu

Na Prince Akbar

MICHUANO ya Ligi Kuu kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kwa msimu wa 2012/2013 itaanza Septemba 15 mwaka huu kwa timu zote 14 kujitupa kwenye viwanja tofauti.

Mechi za ufunguzi zitakuwa kati ya Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Polisi Morogoro vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro), Tanzania Prisons vs Yanga (Sokoine, Mbeya), Mgambo JKT vs Coastal Union (Mkwakwani, Tanga), JKT Ruvu vs Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Kagera Sugar vs Azam (Kaitaba, Bukoba) na Toto Africans vs Oljoro JKT (Kirumba, Mwanza).

Mzunguko wa kwanza (first round) utamalizika Novemba 11 mwaka huu ambapo kwenye mzunguko huo mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itachezwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ligi hiyo itamalizika Mei 18 mwakani kwa mechi kati ya Toto Africans vs Ruvu Shooting (Kirumba), Mgambo JKT vs African Lyon (Mkwakwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Azam Complex), Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Sokoine), Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Azam (Sheikh Amri Abeid Kaluta) na Polisi Morogoro vs Coastal Union (Jamhuri).

Endapo Simba na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho.

Wakati huo huo: Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi rasmi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 kati ya bingwa mtetezi Simba na makamu bingwa Azam itachezwa Septemba 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

SIMBA WATUMA MALALAMIKO TFF KUHUSU TWITE, ILA WAO SASA...YANGA YAPANGUA USAJILI WAO WOTE!

Mbuyu Twite akiwa amevaa jezi yenye jina Rage, baada ya kutua Dar es Salaam jana

Na Prince Akbar

KLABU mbalimbali zimewasilisha pingamizi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga usajili wa wachezaji 17 walioombewa usajili katika timu za Ligi Kuu.

Toto Africans ya Mwanza imewawekea pingamizi wachezaji Enyinna Darlinton aliyeombewa usajili Kagera Sugar, na Mohamed Soud anayekwenda Coastal Union kwa maelezo kuwa bado ina mikataba na wachezaji hao.

Pia Flamingo ya Arusha inapinga usajili wa wachezaji wake Kelvin Friday Iddy katika timu za Azam na Salim Walii (Polisi Mara) kwa vile taratibu za kuwahamisha bado hazijafanywa. Nayo Kagera Sugar inapinga usajili wa beki David Charles Luhende kwenda Yanga kwa vile ada ya uhamisho haijalipwa.

Super Falcon ya Chanjamjawiri, Chakechake, Pemba inapinga wachezaji wake wanne; Edward Christopher Shija, Samir Said Luhava (Simba), Robert Joseph Mkhotya (African Lyon) na Sultan Juma Shija (Coastal Union) kusajiliwa katika timu hizo kwa maelezo taratibu halali za uhamisho hazikufuatwa.

Mchezaji Othman Hassan aliyeombewa usajili Coastal Union anapingwa na Oljoro JKT kwa vile bado ana mkataba na timu hiyo unaomalizika Mei 24, 2013. Nayo Rollingstone Multipurpose Ateclass Foundation ya Arusha inapinga usajili wa Kigi Makassy kutoka Yanga kwenda Simba hadi itakapolipwa fidia ya kumlea mchezaji huyo kwa vile bado hajafikisha umri wa miaka 23.

Azam inapinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba kwa maelezo bado ina mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani. Nayo Simba inapinga Kelvin Yondani kusajiliwa Yanga kwa maelezo kuwa ina mkataba naye uliosainiwa Desemba 23 mwaka jana.

Vilevile Simba imewasilisha malalamiko ya mchezo usio wa kiungwana katika usajili wa Mbuyu Twite aliyeko Yanga kwa maelezo alisaini mkataba na klabu yao Agosti Mosi mwaka huu mbele yao, viongozi wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) na APR ambapo alilipwa dola 30,000 na nyingine 2,000 ikiwa ni fedha ya kujikimu na nauli yake ya kujiunga na klabu hiyo.

Nayo Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu Mbiyavanga na Lino Masombo kwa maelezo walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame. Pia inapinga Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam kwa msimu wa 2012/2013.

Pingamizi lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa kwa maelezo inao wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano. Imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia pingamizi hizo pamoja na usajili wa wachezaji kwa ujumla kwa 2012/2013.

WALIOGOMA KUHESABIWA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI – MBEYA


 Pichani wananchi waliokataa kuhesabiwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bwana Guram Hussein Kifu. katikati ni Kiongozi wa Mgomo Bwana Ally Mwangoto, kutoka dini ya Kiislamu wanaojiita wenye msimamo mkali wakiwa chini ya ulinzi katika mahabusu ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya,wakisubiri kupelekwa Polisi wilayani humo.


Licha ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka waislamu  nchini kushiriki zoezi la Sensa  ya watu makazi, hali hiyo imeonekana kuwa tatizo kwa kijiji cha Ruiwa Kata ya Ruiwa Wilayani Mbarali  ambapo watu wasita wanaosadikiwa kuwa ni waislamu  wenye msimamo mkali kugoma kuhesabiwa  kwa madai  kuwa serikali imepuuza  madai yao.


Imeelezwa kuwa waislamu hao walishaeleza serikali kuwa hawako tayari kuhesabiswa lakini bado serikali imeshindwa kutekeleza matakwa yao na hivyo kukataa kuhesabiwa.


Akizungumza na gazeti hili jana kuhusiana na madai hayo , Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa Bw. Jordan Masweve alisema kuwa kwa kata zoezi la sense toka limeanza imekuwa ni tatizo kubwa sana kutokana na watu hao kuonyesha msimamo wao wa kutotaka kuhesabiwa.


“Wao wanadai kuwa hawapo tayari kuhesabiwa hata iweje msimamo wao ni mmoja hata wafanywe nini lakini suala ni kutokubali kuhesabiwa tu kwa madai serikali imeepuza madai yao toka mwanzo ya kutotaka kuhesabiwa”alisema.


Bw. Masweve alisema tukio hilo limetokea  Agosti 27 mwaka huu majira ya saa 8.30 mchana  katika kijiji cha Ruiwa wakati makarani wa sense  walipofika katika makazi wa wananchi hao  wakiongozwa na Mtendaji wa kijiji  kwa lengo la kuwataka wakubali kuhesabiwa lakini waligoma.


Alisema  hata hivyo zilifanyika jitiha za kuwasihi kushiriki zoezi hilo  lakini hawakutaka kukubali  ndipo mgambo wa kijiji walipowakamata na kuwapeleka kwenye ofisi ya Kata.


Bw. Masweve aliwataja waislamu waliokamatwa kuwa ni Ally Mwangoto,Subeti Juma, Abinala, Pembe ,Ally Suleiman pamoja na Nawab Suleiman licha ya kufikishwa katika ofisi ya kata bado waliendelea kuwa na msimamo wao  kuwa hawako tayari kuhesabiwa na kudai kuwa vyovyote itakavyokuwea wapo tayari  hata kuchinjwa au kufungwa jela lakini si kuhesabiwa.


Hata hivyo alisema kuwa waislamu hao walidai kuwa hata Mkuu wa Wilaya akifika hapo hawako tayari kuhesabiwa msimamo wao ni mmoja tu .


“Bado tupo nao hapa ofisini tukisubiri Mkuu wa Wilaya ya Mbarali ,na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbarali ili waje kuwachukua  watu hawa”alisema.


Aidha aliongeza kuwa kabla ya zoezi hilo kuanza  kulikuwa na mikutano ya  hadhara ambayo ulikuwa unaendeshwa na  viongozi wa kiislamu kutoka Jijini Mbeya  walikuwa wakihamasisha waislamu wenzao kuwa ambao hawatakuwa tayari kushiriki zoezi hilo kukimbilia misikitini ambako watawapelekea chakula mpaka zoezi hilo litakapokuwa limekamilika.


Akizungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kuelekea kijiji cha Ruiwa  Mkuu wa Wilaya Mbarali Bw. Gulamu Hussen Kiffu alisema amepata taarifa za tukio hilo lakini bado hajafika huko lakini yupo njiani kuelekea huko ili aweze kujua undani wa tukio hilo.


“Kwasasa nipo kwenye gari naelekea Ruiwa kwa ajili ya tukio hilo mara baada ya kufika na kuangalia tukio lilivyo nitatoa taarifa kamili na hatua zipi ambazo tutakuwa tumechukua”alisema.


Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Bw.Athuman Diwani alisema bado hajapata taarifa hizo na kudai kuwa taarifa zote za matokeo atatotoa mara baada ya zoezi la sense kumalizika.

Wanafunzi UDSM Waachiwa Huru Na Mahakama



Tausi Ally

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imewaachia huru wanafunzi 51 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kufanya mkusanyiko usio halali na kukaidi amri halali ya askari wa Jeshi la Polisi iliyowataka watawanyike.


Akiwaachia huru wanafunzi hao jana, Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alisema anawaachia huru washtakiwa hao, kwa mujibu wa kifungu cha 225 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA), sura ya 20 kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuliendesha shtaka hilo.


Wanafunzi hao waliachiwa huru baada ya Wakili wa Serikali, Prosper Mwangamila kudai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kubainisha kuwa mahakama ilikwisha toa ahirisho la mwisho Agosti 13, mwaka huu.

Mwangamila alidai kuwa waliwasiliana na mashahidi wao ambao ni askari kupitia kwa RCO wa Wilaya ya Kinondoni ,lakini aliwaambiwa kuwa askari hao ni moja kati ya askari waliopo kwenye Sensa ambayo ni muhimu kama kesi hiyo.

Hivyo Wakili huyo wa Serikali aliiomba mahakama itoe ahirisho lingine la mwisho hadi Jumatatu kwa sababu askari hao bado wapo kwenye Sensa ambayo inaisha Jumapili.


Baada ya kutolewa kwa hoja hizo, Wakili wa Utetezi, Regnal Martin alipinga ombi la kuahirishwa kwa kesi hiyo na kuutaka upande wa mashtaka kuheshimu amri ya mahakama.


Wakili Martin alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo imekuwa ikiahirishwa kwa sababu tofauti ikiwemo ya askari hao kuwepo kwenye mgomo wa madaktari wa Julai 12, mwaka huu.


Akitoa uamuzi juu ya hoja hizo, Hakimu Lema alisema baada ya kupitia mwenendo mzima wa kesi , mahakama inajiuliza swali kuwa mashahidi pekee ni hao hao maaskari na kama ni hao upande wa mashtaka ulipaswa kuwasilisha hati chini ya kifungu cha sheria cha 225 (4) cha CPA ambacho kinaeleza tarabu kama shahidi hayupo nini kifuatwe.

Hakimu Lema alisema sababu zilizotolewa na upande wa mashtaka ni za msingi lakini hazikubaliki na kwamba walichokifanya wameidharau mahakama kwa kutofuata taratibu zilizopo.


Aliongeza kuw ana wasiwasi hata kutoa ahirisho lingine la mwisho kwa upande wa mashtaka kwa sababu akitoa ahirisho hadi Jumatatu wanaweza kwenda na sababu nyingine kuwa askari hao wapo kwenye matukio yaliyotokea baada ya Sensa.


Baada ya kuangalia mwenendo mzima wa kesi hiyo, Hakimu aliliondoa shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 225 (5) sura ya 20 kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuliendesha shtaka hilo.


Wanafunzi walioachiwa huru ni Mwambapa Elias,Evalist Elias, Baraka Monesi, Hellen Mushi, Alphonce Lusako, Matrona Babu, Rolana Wilfred, Godfrey Deogratius , Munisi Denis,Evanos Gumbi pamoja na wenzao 40.


Awali Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya alidai kuwa mnamo Novemba 11 mwaka huu, eneo la Mlimani la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walifanya mkusanyiko usio halali na kusababisha uvunjifu wa amani eneo hilo.


Komanya alidai kuwa washtakiwa hao wakiwa kwenye mkusanyiko huo haramu kwa lengo la kufanya mgomo, askari wa Jeshi la Polisi waliwataka watawanyike, lakini hata hivyo wanafunzi hao walikaidi amri hiyo na kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.


Hata hivyo washtakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, walikana mashtaka hayo na waliachiwa huru baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika ambaye alisaini bondi ya Sh1milioni

Profesa Mbele Na Wanaongoja Ajira Milioni Moja Walizoahidiwa Na CCM!


Huu ni mchango wa Profesa Joseph Mbelea, anasema...

"Ingekuwa bora kama hao wangekuwa maktabani kuliko kupoteza muda wao kwenye kijiwe hiki cha abracadabra. Wangetumia muda wao maktabani wakisoma vitabu na majarida wangekuwa wanajiongezea ujuzi, maarifa, na elimu kwa ujumla. Sio tu ni jambo la manufaa kwa mtu kuelimika, bali pia maandalizi ya ajira.

Kwa mfano, wangetumia muda wao maktaba na kusoma vitabu vya ki-Ingereza, hatimaye wangekuwa na uwezo wa kushindana na wa-Kenya kwenye ajira katika sekta kama utalii. Sekta hii inavyokwenda ni kwamba hata mfagiaji anatakiwa kujua ki-Ingereza kidodo, ili mtalii akiomba shuka au sabuni, aweze kujibiwa.

Lakini hao wa-Tanzania ukiwauliza habari hii ya ajira, wengine watakuambia wanangoja ajira milioni walizoahidiwa na CCM mwaka 2012. Wengine watakuambia serikali ya JK imeshindwa kuwapa ajira. Na kuna siku mhubiri atakuja eneo hili hili na kuwahubiria kuwa wamekosa ajira sababu ya mfumo Kristo. Tena hii abracadabra ya mfumo Kristo imepamba moto kweli.

Inabidi sisi wenye ufahamu wa dunia, kutokana na kutembea sehemu mbali mbali za dunia, na pia kutokana na kusoma, tufanye juhudi ya kuwamegea hao wenzetu elimu ambayo Mungu katupa fursa ya kuipata. Kwa upande wangu, naandika sana kwenye blogu, makala, na hata vitabuni, kuwa dunia ya leo haina mchezo, na njia pekee ya kuimudu na kujipatia mafanikio ni kwa kujielimisha. Ndugu zetu waache kushabikia hizo abracadabra, na badala yake wasome vitabu au kwenda shuleni, kwani. Nyerere alisema elimu haina mwisho, na ndilo fundisho la kuzingatiwa."

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


                                           Release No. 139

                              TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

                                             Agosti 31, 2012

MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI SEPT 27

Mtihani kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Septemba 27 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF. Ada ya mtihani ni dola 50 za Marekani.

Pia Damas Ndumbaro na Ally Mleh wa Manyara Sports Management ambao tayari ni mawakala wanaotambuliwa na FIFA wanatakiwa kufanya mtihani huo kama wanataka kuendelea na uwakala kwa vile muda wa leseni zao za awali umemalizika.

Mawakala wengine ambao ni John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully leseni zao bado ziko hai.

WACHEZAJI 17 WAPINGWA KWENYE USAJILI

Klabu mbalimbali zimewasilisha pingamizi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupinga usajili wa wachezaji 17 walioombewa usajili katika timu za Ligi Kuu.

Toto Africans ya Mwanza imewawekea pingamizi wachezaji Enyinna Darlinton aliyeombewa usajili Kagera Sugar, na Mohamed Soud anayekwenda Coastal Union kwa maelezo kuwa bado ina mikataba na wachezaji hao.

Pia Flamingo ya Arusha inapinga usajili wa wachezaji wake Kelvin Friday Iddy katika timu za Azam na Salim Walii (Polisi Mara) kwa vile taratibu za kuwahamisha bado hazijafanywa. Nayo Kagera Sugar inapinga usajili wa beki David Charles Luhende kwenda Yanga kwa vile ada ya uhamisho haijalipwa.

Super Falcon ya Chanjamjawiri, Chakechake, Pemba inapinga wachezaji wake wanne; Edward Christopher Shija, Samir Said Luhava (Simba), Robert Joseph Mkhotya (African Lyon) na Sultan Juma Shija (Coastal Union) kusajiliwa katika timu hizo kwa maelezo taratibu halali za uhamisho hazikufuatwa.

Mchezaji Othman Hassan aliyeombewa usajili Coastal Union anapingwa na Oljoro JKT kwa vile bado ana mkataba na timu hiyo unaomalizika Mei 24, 2013. Nayo Rollingstone Multipurpose Ateclass Foundation ya Arusha inapinga usajili wa Kigi Makassy kutoka Yanga kwenda Simba hadi itakapolipwa fidia ya kumlea mchezaji huyo kwa vile bado hajafikisha umri wa miaka 23.

Azam inapinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba kwa maelezo bado ina mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani. Nayo Simba inapinga Kelvin Yondani kusajiliwa Yanga kwa maelezo kuwa ina mkataba naye uliosainiwa Desemba 23 mwaka jana.

Vilevile Simba imewasilisha malalamiko ya mchezo usio wa kiungwana katika usajili wa Mbuyu Twite aliyeko Yanga kwa maelezo alisaini mkataba na klabu yao Agosti Mosi mwaka huu mbele yao, viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na APR ambapo alilipwa dola 30,000 na nyingine 2,000 ikiwa ni fedha ya kujikimu na nauli yake ya kujiunga na klabu hiyo.

Nayo Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu Mbiyavanga na Lino Masombo kwa maelezo walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame. Pia inapinga Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam kwa msimu wa 2012/2013.

Pingamizi lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa kwa maelezo inao wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano. Imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia pingamizi hizo pamoja na usajili wa wachezaji kwa ujumla kwa 2012/2013.

LIGI KUU TANZANIA BARA 2012/2013

Michuano ya Ligi Kuu kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kwa msimu wa 2012/2013 itaanza Septemba 15 mwaka huu kwa timu zote 14 kujitupa kwenye viwanja tofauti.

Mechi za ufunguzi zitakuwa kati ya Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Polisi Morogoro vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro), Tanzania Prisons vs Yanga (Sokoine, Mbeya), Mgambo JKT vs Coastal Union (Mkwakwani, Tanga), JKT Ruvu vs Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Kagera Sugar vs Azam (Kaitaba, Bukoba) na Toto Africans vs Oljoro JKT (Kirumba, Mwanza).

Mzunguko wa kwanza (first round) utamalizika Novemba 11 mwaka huu ambapo kwenye mzunguko huo mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itachezwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ligi hiyo itamalizika Mei 18 mwakani kwa mechi kati ya Toto Africans vs Ruvu Shooting (Kirumba), Mgambo JKT vs African Lyon (Mkwakwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Azam Complex), Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Sokoine), Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Azam (Sheikh Amri Abeid Kaluta) na Polisi Morogoro vs Coastal Union (Jamhuri).

Endapo Simba na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho.

MECHI YA UFUNGUZI WA MSIMU WA LIGI 2012/2013

Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi rasmi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 kati ya bingwa mtetezi Simba na makamu bingwa Azam itachezwa Septemba 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

SERENGETI BOYS KUJIPIMA KWA ASHANTI

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) iliyokuwa kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Kenya itavunja rasmi kambi yake kesho (Jumamosi) kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Ashanti United.

Mechi hiyo dhidi ya Ashanti United iliyoko daraja la kwanza itachezwa kuanzia saa 10 jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kwa kiingilio cha sh. 2,000.

Serengeti Boys ilikuwa Septemba 9 mwaka huu icheze na Kenya kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, lakini Kenya ikajitoa ambapo sasa itacheza na Misri katika raundi ya pili. Mechi ya kwanza itachezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwishoni mwa Septemba, Serengeti Boys itarejea tena kambini kujiandaa kuikabili Misri ambapo kabla inatarajia kupata mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu itakayotangazwa baadaye.

MCHEZAJI WA MTIBWA SUGAR NAYE APATA ITC

Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) limetuma Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Ayoub Hassan Isiko aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea timu ya Bull FC ya nchini humo.

ITC hiyo ilitumwa jana (Agosti 30 mwaka huu), hivyo kufanya wachezaji ambao ITC hazijapatikana hadi sasa kubaki wawili tu. Dirisha la usajili wa wachezaji litafungwa rasmi Septemba 4 mwaka huu.

Wachezaji ambao ITC zao bado hazijapatikana ni Salum Kinje na Pascal Ochieng kutoka AFC Leopards ya Kenya waliojiunga na Simba. ITC hizo zinatarajiwa kupatikana wakati wowote kwani tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeshaziomba kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) baada ya nyaraka zote zilizokuwa zikitakiwa kupatikana.

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

JICHO LETU KATIKA MAGAZETI AUG 31

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.



0
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

POLISI MANYARA WAPIGA, WATESA NA KUJERUHI VIBAYA MTOTO, WALIMBANA SEHEMU ZA SIRI HADI AKAPOTEZA FAHAMU


Mtoto aliyepigwa na askari polisi hadi kupoteza fahamu,Kadogoo Kalanga(16)mkazi wa Orkesmet Wilayani Simanjiro akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi(ICU) ndani ya hospitali ya Selian akiwa anahudumiwa na manesi hospitalini hapo juzi jijini Arusha

  • WAMSHAMBULIA KWA MARUNGU NA KUMBANA SEHEMU ZAKE ZA SIRI HADI KUTOKWA NA HAJA NDOGO.

  • APOTEZA FAHAMU NA KULAZWA WODI YA WAGONJWA MAHUTUTI.

JESHI la Polisi Mkoani Manyara limeingia katika shutuma nzito baada ya Askari wake wa tatu kutuhumiwa  kumpiga mtoto mwenye umri wa miaka 16 wa jamii ya kifugaji anayejulikana kwa jina la Kadogoo Kalanga mkazi wa Orkesmet Wilayani Simanjiro hadi kupoteza fahamu.

Tukio hilo lilitokea Jumatatu Agosti 28, 2012  majira ya saa tano na nusu katika eneo la Orkesmet ambapo askari watatu mmoja wao akitambulika kwa jina moja tu la John walimkamata mtoto huyo mara baada ya kumtuhumu kuiba mbuzi wa jirani yake ambaye anajulikana kama Mama Shedi mkazi wa eneo hilo la Orkesmet.

Mmoja wa ndugu wa kijana huyo akiwa anawaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani nguo(kaptula) ya kijana aliyepigwa na askari polisi hadi kupoteza fahamu namna ilivyokuwa imechanika chanika baada kushushiwa kipigo

Mashuhuda wanadai kuwa polisi hao baada ya kumkamata mtoto huyo, walianza kumuadhibu bila huruma hali iliyopelekea mtoto huyo kulazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Selian iliyopo jijini Arusha.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa hakuna jarida lolote lililofunguliwa kutokana na kisa hiki. Watu wakaribu na mtoto huyu wanadai kuwa walitaka kufungua mashtaka dhidi ya askari waliofanya unyama huo lakini walikataliwa.


MAMA MZAZI WA KIJANA KADOGOO KALANGA AMBAYE ALIPIGWA NA MAASKARI WA KITUO CHA OLKESIMETI AKIWA ANAONYESHA SEHEMU AMBAZO MTOTO WAKE ANAMAUMIVU MAKALI  BAADA YA KUPIGWA

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ndani ya Hospitali ya Selian  mama mzazi  wa kijana huyo, Bi. Paulina Kalanga alisema kwamba askari hao watatu walimfuata kijana wake eneo la mnadani na kumtuhumu kuiba mbuzi na kuanza kumshumbulia kwa kumpiga bila kumpa nafasi ya kujitetea kitendo kilichopelekea kuanza kutokwa na haja ndogo mfululizo na kisha kupoteza fahamu.

“Yaani walimkamata kijana wangu kisha wakaanza kumpiga kwa marungu na mateke ….. wakazishika sehemu zake za siri na kuanza kugongagonga na kitako cha silaha ya moto ndipo alipoanza kujikojolea mfululizo na kupoteza fahamu”alisema huku machozi yakimtiririka


WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA SELIANI WAKIWA WANAMUHAMISHA HOSPITALI  MTOTO HUYO  BAADA YAKUKOSA KIFAA CHA KUMPIMIA KATIKA HOSPITALI HIYO NA KUMPELEKA  HOSPITALI YA AGAKAN

Taarifa zinasema kuwa polisi  hao baada ya kuona hali ya mtoto huyo imekuwa mbaya walimbeba na kisha kumkimkimbiza haraka katika kituo cha afya cha Orkesmet kwa ajili ya matibabu kabla ya wanandugu kuomba gari la wagonjwa mahututi (ambulance) kumkimbiza katika hospitali ya Selian iliyopo mkoani Arusha.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara, Akili Mpwapwa alipohojiwa juu ya tukio hilo alikiri kupata taarifa zake  huku akisema kwa kifupi kwamba tayari ameshatoa maelekezo kwa mkuu wa polisi wilayani humo kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na kisha aletewe ripoti kamili mezani kwake.

“Nimeshatoa maelekezo kwa OCD kwamba uchunguzi wa kina ufanyike na nipewe ripoti kamili kwa kuwa jana ndiyo nilipigiwa simu na kuelezwa juu ya tukio hilo”alisema

Hatahivyo,aliongeza kwa kusema kwamba endapo kuna askari atabainika kuhusika na tukio hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

“Ikibainika askari amehusika basi hatua kali za kisheria  zitachukuliwa na hapa tayari uchuinguzi unaendelea”alisema

KADA CHADEMA APIGWA, KUNG’OLEWA MENO

KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika tawi jipya la Misongeni, mjini hapa, Emmanuel Constantine, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa CCM.

Katika tukio hilo lililotokea juzi saa 12 jioni, Emmanuel ambaye amefungua jalada polisi Agosti 28, mwaka huu, aling’olewa meno mawili ya juu na kuumizwa sehemu mbalimbali za mwili.

Gazeti hili lilifika katika wodi namba moja ya Hospitali ya Rufaa mjini hapa ambapo kada huyo amelazwa na kuelezwa na mashuhuda kuwa watu hao wakiwa na fimbo na makopo ya rangi, waliing'oa bendera ya CHADEMA kwenye jiwe lililozinduliwa juzi na kisha kulipaka rangi nyingine jiwe hilo.

“Ilipofika saa 12 jioni wakatokea hao jamaa wa CCM wakiwa na fimbo na makopo ya rangi, wakaing'oa bendera na kuitupa kisha wakaanza kupaka rangi walizokuwa nazo, Emmanuel akawasogelea na kuwauliza kwanini wanafanya hivyo, ndipo wakamgeukia na kuanza kupiga,” alisema shahidi aliyejitambulisha kwa jina la Innocent.

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani hapa, Zuberi Kiloko, aliyefika eneo hilo baada ya kada huyo kujeruhiwa, alisema kuwa alimkuta Emmanuel akiwa hajitambui na kulazimika kukodi gari ili kumkimbiza hosipitali.

“Ingawa kulijitokeza usumbufu wa kupata PF3, tunashukuru kuwa hatimae tuliipata na mgonjwa ametibiwa kwa kuwekwa nyaya mdomoni na kushonwa nyuzi sita kwenye taya...ameruhusiwa kurudi nyumbani,” alifafanua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alikana kuwa na taarifa hiyo, huku akisema matukio kama hayo ni mengi sana hivyo hawezi kufahamu labda ni walevi waligombana vilabuni.

CHAVITA YAZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUWAPA MGAO WAO WA FEDHA ZA WALEMAVU WENYE VVU

CHAMA cha Viziwi Tanzania Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kimeitaka Halmashauri ya wilaya hiyo kutoa fedha zinazotengwa na serikali kwa ajili ya mfuko wa walemavu wa Ukimwi.

Hayo yamebainishwa  na Mratibu wa mradi wa mafunzo yalugha ya alama Wilaya Kondoa Mustaph Shabani, kwenye mafunzo ya lugha ya alama yaliyofadhiliwana shirika la The Foundation for Civic Society (FCS)
kwa ajili ya watumishi wataasisi mbalimbali za kiserikali iliyofanyika Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma.

Shabani amesema chama cha viziwi kinashangazwa kuona Halmashauri hiyo ikishindwa kuwapatia fedha hizo ambazo zimekuwazikitengwa na serikali kila mwaka kwa ajili ya maendeleo ya walemavu.

Amesema Chavita inatambua serikali kwa kupitia Halmashauri zake hapa nchini imekuwa zikitenga fungu hilo kwa ajiliwalemavu lakini Katibu Tawala wa Wilaya ya Kondoa Dorosta Katokwa upande wake aliwataka watumishi wa idara ya Afisa Maendeleo na Jamii naAfisa

Maendeleo ya Jamii walifikishe suala hilo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kama kuna fungu hilo kwa ajili ya jamii wasiojiweza.

Dorosta amesema fungu hilo kama lipo kwa Mkurugenzi nihaki yao hivyo hakuna sababu ya kutolifuatilia wakati viziwi hao wanamahitajimengi wanayokabiliana nayo yakiwemo ya ugonjwa wa ukimwi.

Kwea upande wao wazazi na Walezi wa watoto wenye ulemavu wa kutosikia (viziwi) wameomba mradi wa mafunzo ya lugha ya alama unaofadhiriwa na shirikalisilo la kiserikali la the Foundation for Civic Society, kuwapatia mafunzoya muda mrefu yatakayo warahisishia uwelewa zaidi wa elimu ya mawasiliano pindiwanapokuwa na

familia zao.

Mmoja wa wazazi haoFatuma Raffa alisema wametoa ombi hilo kutokana na muda unaotolewa wa mafunzo ya lugha ya alama kuwa mdogo kwa kuwa wazazi walio wengi hawana elimuya uwelewa wa mawasiliano

Usafiri wa reli wamchanganya Dk. Mwakyembe



Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amesma sekta ya usafiri wa reli nchini inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo gharama kubwa za uendeshaji, kutoaminika, huduma duni, sheria, sera na mifumo ya udhibiti kutokana na kutokuwepo na uwekezaji wa kutosha usiokuwa na ushindani.

Dk. Mwakyembe alisema hayo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa watalaamu wa sekta ya usafiri wa reli uliokuwa ukijadili rasmu ya sera ya reli nchini ambao ulifanyika jana jijini Dar es Salaam.

Dk. Mwakyembe alisema ili kurejesha sekta ya reli kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, serikali imeamua kuandaa sera ya reli itakayojitegemea badala ya hivi sasa ambapo ipo sera ya uchukuzi ambayo ni pana na inajumuisha mambo mengi.

Alisema miongoni mwa mambo ambayo yanatakiwa kuangaliwa na wataalam hao ni kuona kama Tanzania tuwe na reli ya upana upi, kwani iliyopo ina upana wa mita moja.

Aliongeza kuwa baadhi ya wadau wanaona kwamba upana wa mita moja ni kama umepitwa na wakati japo zipo nchi kama Japana na nchi nyingine barani Afrika zinazotumia reli yenye upana huo.

Dk. Mwakyembe alisema hata kwa nchi za Afrika Mashariki zinahitaji kuwa na mfumo wa reli zenye upana mmoja ambazo ni mita 1.435 ambayo inatumiwa na nchi nyingi duniani.

Alisema kwa nchi kubwa kama Tanzania yenye idadi ya takribani watu milioni 40 kunahitaji kuwa na usafiri wa reli wa uhakika ambao ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Alisema katika kuhakikisha sekta ya usafiri wa reli inaboreshwa, serikali ipo katika mchakato wa kununua vichwa 13 vya treni na vingine 18 vya kukodishwa.

Hata hivyo, Dk. Mwakyembe alisema kukodisha vichwa vya treni imekuwa ghali sana hivyo serikali inalenga kufufua vichwa vibovu vilivyopo nchini kwa kuhakikisha mafundi wanafanya kazi hiyo usiku.

Mwenyekiti wa kamati iliyopewa jukumu la kutayarisha rasmu ya kutengeneza sera ya reli, Dk. Malima Bundara, alisema wakati wa kutembelea mikoa mbalimbali walibaini hali ya usafiri wa reli ni mbaya na miundombinu yake imechakaa sana.

Dk. Bundara alisema changamoto nyingine walizobaini ni kuvamiwa kwa njia za reli na uwekezaji hivyo kuna haja ya kuwa na miongozo kama serikali katika kuboresha usafiri huo.