Mtoto wa miaka 8 atiwa Meno na Mama yake mzazi.

Na John Banda, Dodoma

MTOTO Magge Fred 8 amejeruhiwa kichwani na kung'atwa kwa meno Mgongoni na mabegani na Mama yake mzazi kwa sababu aliiba fedha na kununulia Chips bila ruhusa.

Magge alisema anajisikia maumivu makali kichwani na mgongoni baada ya kupigwa na mama yake mzazi kutokana na madai ya yeye kutomwambia Dada yake alipo na chips ambazo mama yake alizikuta chini ya mvungu wa kitanda


tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jumanne hii, inadawa kuwa Theresia Fidelis ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo alimpiga na kumjeruhi mwanae, mwandishi wetu alishuhudia kovu kichwani la kipigo cha kitu kilichomchana na huku mgongoni kukiwa na majeraha kadha ya meno ambavyo vimemsababishia maumivu makali.


Akiongea mbele ya Mwenyekiti wa mtaa mama wa mtoto huyo alisema aliamua kumpiga kiasi hicho kutokana na mtoto huyo kumfichia siri Dada yake na pia kuiba fedha ndani na kununua chipsi pamoja na matumizi mabaya ya anasa.

Theresia alisema imekuwa ni kawaida kwa mtoto wake huyo Magge Fred 8  kutosema Dada yake alipo na fedha zinazopotea ndani kutojulikana aliyechukua badala yake anaona chipsi na vitu vingine vidogo vidogo vya anasa ndiyo sababu ya kumpiga vibao mpaka kujigonga ukutani na kuchanika kichwani na kumng'ata kutokana na hasira.

.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume kata ya Mnadani Matwiga Kyata alisema tukio hilo lililpofikishwa ofisini kwake aliamua kuchukua hatua za kisheria na baada ya mahojiano aliamua kuwaita polisi ili sheria ikachukue mkondo wake zaidi.

Baadhi ya akina mama waliokuwepo ofisini hapo kushuhudia tukio hilo walisema mtoto huyo alikimbia toka kwa nyumbani kwao usiku huku akilalama kutaka kuuawa ndipo waka mpeleka kwa mwenyekiti, pamaja na kulaani kitendo alichofanya mwanamke mwenzao.

''We acha hivi unajua uchungu tunaoupata wakati wa kujifungua? kama kweli aliupata angeweza kufanya hivi mpaka kufikia kumng'ata meno akitaka kumnyofoa nyama mtoto wake wala haiingii akili labda akapimwe akili la sivyo achukuliwe hatua kali zinazostahili'', alisema Mwatum Rashid.

Polisi walithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi wanapoona watoto wakifanyiwa vitendo viovu na wazazi au walezi  wao.