Mwimbaji wa injili Msomali ndani ya tamasha la Xmas Dodoma







 Mwimbaji wa nyimbo za injili Toka nchini SomaliaMARY SINKALA atakaeshiriki katika tamasha la kristmas litakalofanyika Dodoma Des 25 ndani ya uwanja wa jamhur

Na John Banda, Dodoma
Waimbaji wa nyimbo za injili watakaotumbuiza katika Tamasha la kusifu [Shangwe za Xmas] Dodoma kutoka Nje ya nchi waendelea kuongezeka. Ni Baada ya mwimbaji kutoka Nchini Kenya TUMSIFU RUFUTU mwimbaji wa wimbo wa Mwambie Farao kuwa rasmi kwenye tamasha la Kristmas litakalofanyika Dodoma Tar 25.12.2013 katika uwanja wa Jamhuri, Hatima mwingine aongezeka kutoka nchini Somaria Bi. MARY SINKALA mwenye wimbo wa "Mkumbuke Muumba wako". Tayali waimbaji hao wote wameshawataka wakazi wote wa mkoa huo na vitongoji vyake na watakaotoka nje kujiandaa kwani wao wamejiandaa vya kutosha na kwamba watawafundisha namna ya kumkumbuka muumba wao na
jinsi ya kuelekea kaanani. Shangwe hizo ambazo kwa sasa ni gumzo mkoani humo kutokana na kuandaliwa kwa umahili mkubwa na kampuni ya Liberty Promotion Company ya mjini humo tayali wakurugenzi wake wamewataka watu kuhudhuri kwa wingi kutokana na kiingilio  kidogo kitakachomuwezesha kila mtu kukimudu cha 2000 kwa wakubwa na watoto 1000. Kampuni hiyo imesema Dodoma imekuwa nyuma kwa muda mrefu hasa nyakati
za Sikukuu za kidini na hivyo wamekusudia kukata kiu za wananchi
mkoani humo kwa shangwe za kumuimbia na kumtukuza mungu kupitia matamasha ya mara kwa mara kuanzia  KRISTMAS ya mwaka huu, huku wakiahidi kuibua vipaji vya chipukizi wengi.
Tamasha hilo litawaunganisha waimbaji toka ndani na nje ya nchi  hasa wa mikoa ya DSM na Dodoma itakayobebwa na waimbaji toka makanisa mbalimbali na wanachuo wa chuo kikuu cha Dodoma [UDOM]