Raia wa Japan leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Hiroshima.
Takriban watu laki moja na arobaini walikadiriwa kupoteza maisha baada ya Ndege ya Marekani kudondosha bomu ambalo liliuharibu mji huo tarehe 6 mwezi Agosti mwaka 1945.
Watu elfu sabini walipoteza maisha papo hapo, huku wengine wa idadi kama hiyo walipoteza maisha kutokana na athari za mionzi ya sumu.
Katika hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alisema kumbukumbu ya Heroshima inasisitiza uhitaji wa kufanya jitihada ya kupiga vita matumizi ya Nuklia.
Shambulio la Hiroshima lilifuatiwa na shambulio jingine la bomu la Atomiki katika mji wa Nagasaki.
Japan ilijisalimisha siku kadhaa baadae, hatua iliyomaliza vita ya pili ya dunia.
No comments:
Post a Comment