Pemba: Zaidi ya tani mbili za bidhaa za vyakula
,vinywaji na mafuta zilizokamatwa kutoka maduka tofauti kwa kumalizika
muda wake wa matumizi vitachomwa moto.
Bidhaa hizo zitateketezwa na
Idara ya Biashara ya Wizara ya Biashara , Viwanda na Masoko Pemba katika
eneo la Kwareni , Vitongoji mko wa Kusini Pemba.
Ofisa Idara ya Biashara wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Pemba,
Mussa
Omar Issa alisema bidhaa hizo zimepatikana kufuatia msako uliofanywa na
watendaji wa idara hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi kwenye
maduka Kisiwani Pemba .
Alisema katika msako huo uliofanyika kwenye
maduka ya chakula na vinywaji wamebaini kuwepo na taaluma ndogo kwa
jamii kuhusiana na matumizi ya vyakula ambavyo vimepita muda wa matumizi
yake .
“Msako huu tulioufanya utakuwa endelevu
,ambapo lengo lake ni kuwalinda walaji juu ya utumiaji wa vyakula
vilivyopita muda wa matumizi yake ,kwani tumebaini kwamba bado jamii ina
hitaji elimu ya kutosha kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema
Alisema kuwa katika msako huo mfanyabiashara
alipewa fomu na kujaza pamoja na kulipia nusu ya gharama kutokana na
bidhaa zilizobainika kuwa zimepita muda wa matumizi .
No comments:
Post a Comment