Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka.
Dar es Salaam. Vigogo watatu wa
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne, ikiwamo
la matumizi mabaya ya madaraka, ufujaji na ubadhirifu wa fedha na wizi
wa Sh200 milioni.
Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu
Mkazi, Aloyce Katemana, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliwataja washtakiwa hao
kuwa ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sera na Mipango, Simon Lazaro,
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa Ardhi, Mipango na Matumizi, Gerald
Mango na Kaimu Mhasibu Mkuu wa NLUPC, Charles Kijumbe.
Katika shtaka la kwanza linalomkabili Simon, Swai
alidai kuwa Novemba 17, 2012 katika ofisi za Kamishna wa Ardhi,
Mipango na Matumizi iliyopo Wilaya ya Ilala aliwasilisha nyaraka za
marejesho ya matumizi ya fedha kwa Mkurugenzi w wa Tume ya Ardhi Mipango
na Matumizi akionyesha Sh100 milioni zilipokelewa kwa ajili ya matumizi
ya mipango na matumizi ya ardhi wilaya za Babati, Kilolo na Bariadi
wakati akijua kuwa siyo kweli.
Swai alidai katika shtaka la pili, washtakiwa wote
kati ya Julai 2011 na Agosti 5, 2011 wakiwa waajiriwa wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, walitumia madaraka yao vibaya
kinyume na kanuni ya 87 (1) na 86(1) ya Sheria ya Udhibiti wa Fedha za
Umma ya 2004.
Katika washtakiwa walikana mashtaka yote yanayowakabili, Hakimu Katemana aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 30, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment