Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari...!
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 16, 2012
SIMBA YAANZIA RAUNDI YA NANE KWA KAGERA SUGAR
Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi
nane kesho (Oktoba 17 mwaka huu) kwa mechi tano huku vinara wa ligi hiyo
Simba wakiialika Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
hiyo namba 52 itachezeshwa na mwamuzi Ronald Swai kutoka Arusha wakati
waamuzi wasaidizi ni Julius Kasitu na Methusela Musebula, wote kutoka
Shinyanga.
Mwamuzi
wa akiba ni Ephrony Ndisa wa Dar es Salaam huku mtathimini wa waamuzi
akiwa Charles Mchau kutoka Moshi.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi
kati ya Tanzania Prisons inayofundishwa na Jumanne Chale na Azam iliyo
chini ya kocha Boris Bunjak kutoka Serbia. Nayo Polisi Morogoro
iliyopanda msimu huu itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa
Jamhuri.
Mgambo
Shooting ambayo imepata ushindi mara mbili mfululizo itakuwa nyumbani
Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga ikiikaribisha Toto Africans katika
mechi itakayochezeshwa na Geofrey Tumaini wa Dar es Salaam. Oljoro JKT
inayonolewa na Mbwana Makata itakuwa nyumbani Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha dhidi ya African Lyon.
LIGI
DARAJA LA KWANZA KUANZA OKTOBA 24
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ya Tanzania Bara inaanza rasmi
Oktoba 24 mwaka huu kwa timu 18 kati ya 24 kujitupa kwenye viwanja tisa
tofauti katika ligi hiyo inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Mechi
za raundi ya kwanza za kundi A zitakazochezwa Oktoba 24 mwaka huu ni
Burkina Faso dhidi ya Mbeya City (Jamhuri, Morogoro), Mlale JKT na Small
Kids (Majimaji, Songea) na Kurugenzi Mufindi dhidi ya Majimaji (Uwanja
wa Wambi, Mufindi mkoani Iringa).
Mkamba Rangers na Polisi Iringa zitakamilisha raundi ya kwanza kwa kundi
hilo Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mechi
za raundi ya pili kwa kundi hilo zitachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwa
Polisi Iringa vs Mbeya City (Samora, Iringa), Majimaji vs Small Kids
(Majimaji, Songea), Burkina Faso vs Mkamba Rangers (Jamhuri, Morogoro)
na Kurugenzi Mufindi vs Mlale JKT (Wambi, Mufindi).
Raundi
ya tatu ni Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Mbeya City vs Mlale
JKT (Sokoine, Mbeya), Small Kids vs Mkamba Rangers (Nelson Mandela,
Sumbawanga), Majimaji vs Burkina Faso (Majimaji, Songea) na Polisi
Iringa vs Kurugenzi Mufindi (Samora, Iringa).
Kundi
B Oktoba 24 mwaka huu ni Ndanda vs Transit Camp (Uwanja wa Nangwanda
Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Moro United (Mabatini, Pwani) wakati
Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors vs Tessema (Mabatini, Pwani) na
Polisi Dar es Salaam vs Ashanti United (Chamazi, Dar es Salaam).
Raundi
ya pili kwa kundi hilo ni Oktoba 27 mwaka huu Ndanda vs Green Warriors
(Nangwanda Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Tessema (Mabatini, Pwani)
wakati Oktoba 28 mwaka huu ni Ashanti United vs Transit Camp (Mabatini,
Pwani) na Oktoba 29 mwaka huu ni Moro United vs Polisi Dar es Salaam
(Chamazi, Dar es Salaam).
Novemba
1 mwaka huu ni Green Warriors vs Ashanti United (Mabatini, Pwani),
Novemba 2 mwaka huu ni Polisi Dar es Salaam vs Villa Squad (Chamazi, Dar
es Salaam), Novemba 4 mwaka huu ni Tessema vs Ndanda (Chamazi, Dar es
Salaam) na Transit Camp vs Moro United (Mabatini, Pwani).
Kundi
C ni Oktoba 24 mwaka huu Kanembwa FC vs Polisi Dodoma (Lake Tanganyika,
Kigoma), Mwadui vs Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi Mara
(Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi,
Tabora).
Raundi
ya pili ni Oktoba 27 mwaka huu; Polisi Tabora vs Polisi Dodoma (Ali
Hassan Mwinyi, Tabora), Mwadui vs Polisi Mara (Kambarage, Shinyanga),
Kanembwa FC vs Morani (Lake Tanganyika, Kigoma) na Pamba vs Rhino
Rangers (Kirumba, Mwanza).
Oktoba 31 mwaka huu ni raundi ya tatu; Polisi Mara vs Rhino Rangers
(Karume, Musoma), Morani vs Polisi Tabora (Kiteto, Manyara), Polisi
Dodoma vs Pamba (Jamhuri, Dodoma) na Kanembwa FC vs Mwadui (Lake
Tanganyika, Kigoma).
MBAGA
AZICHEZESHA KENYA, BAFANA BAFANA
Mwamuzi Oden Mbaga wa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA) ndiye anayechezesha mechi ya kirafiki kati ya
Kenya (Harambee Stars) na Afrika Kusini (Bafana Bafana).
Mechi hiyo inachezwa leo Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini
Nairobi. Mbaga anasaidiwa na waamuzi wasaidizi wa FIFA, John Kanyenye
kutoka Mbeya na Erasmo Jesse wa Morogoro.
TFF
imeteua waamuzi hao baada ya kupata maombi kutoka kwa Shirikisho la
Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) ambao ndiyo waandaaji wa mechi hiyo ambayo
ni moja ya vipimo kwa kocha mpya wa Harambee Stars, Henry Michel kutoka
Ufaransa.
TAFCA
YAONGEZA MUDA WA KUCHUKUA FOMU
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania
(TAFCA) imeongeza muda kwa wagombea kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi
wa chama hicho ambao sasa utafanyika Novemba 25 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan
Mambosasa, jana ndiyo ilikuwa mwisho wa kuchukua fomu lakini mwitikio wa
wagombea bado umekuwa mdogo ambapo ni watano tu waliojitokeza.
Hivyo,
amesema wameongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu ambapo mwisho
itakuwa ni Oktoba 19 mwaka huu saa 10 kamili alasiri.
Fomu
zinapatikana ofisi za TAFCA ambazo ziko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Dar es Salaam.
Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu,
Katibu Msaidizi, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, Mhazini na wajumbe
watatu wa Kamati ya Utendaji.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF
No comments:
Post a Comment