Niliwahi
kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali
imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza
kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama
chama cha mauaji. Raia watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na
mmoja amefariki. Haya yamefanyika kwenye maandamano ya amani ya wananchi
kuwapokea viongozi wa CHADEMA kuelekea kwenye mkutano. Vurugu
zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video.
Vyanzo vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za
kuwasha toka Dar Es Salaam. Tuombe MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa
hadhara ambao wananchi wamekusanyika kwa wingi hivi sasa. States
captured by grand corruption of the ruling party cronies for so many
years resorts to bullets as a way of stopping M4C through the ballot.
Maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya
wengi.
John John MNYIKA,
27 Agosti, 2012
No comments:
Post a Comment