Asilimia kubwa ya raia wa Uingereza wamepiga kura ya maoni wakiitaka ijiondoe kwenye muungano wa bara Ulaya EU.
Huku
asilimia kubwa ya kura zikiwa zimekwisha hesabiwa, asilimia 52% ya raia
wa Uingereza wamepiga kura ya kumaliza uanachama wa Uingereza ndani ya
EU uliodumu miaka 43.
Watu wanaoishi katika mji London na Scotland ndio waliopiga kura kwa wingi kusalia ndani ya muungano huo.
Wandani wa maswala ya afisi ya waziri mkuu bwana David Cameron,wanasema kuwa sasa Britain imeingia katika eneo jipya.
Wadadisi
wa maswala ya kisiasa wanahofu athari za kujiondoa kwa Uingereza kwenye
muungano huo utabainika katika masoko ya hisa huku kukitarajiwa athari
kubwa kiuchumi kisiasa ndani na nje ya bara Ulaya
Sarafu ya Euro
imepanda katika masoko ya fedha huku Paundi ya Uingereza ikiendelea
kuporomoka ikiwa ni ishara kuwa wafanyabiashara wanatarajia Uingereza
kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya.
Kwa mujibu wa ripoti waliojitokeza kupiga kura hiyo ya maoni inaonyesha kuwa wengi.
Hadi
sasa ni majimbo machache ndio hayametangaza matokeo yao na inaonyesha
mchuano ni mkali kati ya wanaotaka kubakia na wale wanaotaka Uingereza
kujiondoa ndani ya Umoja huo wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment