Waasi wa M23 watishia kususia mazungumzo
Waasi wa M23
Mazungumzo ya kuleta amani kati
ya kundi la M23 na serikali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo yanarejelewa tena hii leo mjini Kampala Uganda.
Mazungumzo hayo yalisitishwa mwaka jana kwa ajili ya sherehe za Krismasi na mwaka mpya.
Hata
hivyo vigogo husika kwenye mzozo huo,Rais Joseph Kabila na Jean Marie
Runiga kiongozi wa kundi hilo la waasi wa M23 hawatahudhuria mazungumzo
hayo.
Kundi hilo la M23 limetishia kujiondoa kwenye
mazungumzo hayo hadi pale rais Joseph Kabila atakaposaini mkataba wa
kusitisha mapigano.
Msemaji wa serikali ya Congo ameliambia shirika
la Habari la Reuters kuwa limepuuza masharti hayo ya waasi kwa kuwa
hayana msingi wowote.
Mazungumzo ya kujaribu kutatua mzozo huo
uliodumu kwa zaidi ya miezi tisa yaliyofanyika mwaka uliopita
yalisambaratika, baada ya wawakilishi wa pande hizo mbili kushindwa
kuafikiana.
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu laki nane
wamekimbia makwao tangu waasi hao kaunzisha vita dhidi ya serikali ya
nchi hiyo mwezi Mei Mwaka uliopita, kwa tuhuma za kupuuza mkataba
uliokuwa sainiwa awali wa kuwashirikisha katika jeshi la serikali.
Waasi wadai kutaka kuimarisha hali ya maisha
Jean-Marie Runiga
Waasi hao ambao wanaongozwa na Bosco Ntaganda,
ambaye anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita ICC, kwa
madai ya uhalifu wa kivita, wamepiga hatua kubwa tangu mwaka uliopita.
Waasi hao waliuteka mji wa Goma, mwezi Novemba lakini walijiondoa kufuatia shinikizo za kimataifa.
Kiongozi wa shughuli za kisiasa wa waasi hao,
Jean-Marie Runiga, aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali ya
Congo, haikuwa imetimiza mapendekezo yake ya kusitisha mapigano na kuwa
wanajeshi wa serikali wamekuwa wakijiandaa kuwashambulia.
Kundi hilo la M23 limeshutumiwa na Umoja wa
mataifa kwa kufanya maasi dhidi ya raia jambo ambalo kiongozi wake Jean
Marie Runiga amekanusha.
M23 imesema iataka kuimarisha hali ya maisha ya
watu wa Mashariki mwa Congo, lakini Umoja wa Mataifa umedai kuwa waasi
hao wanaungwa mkono na serikali za Rwanda na Uganda, madai ambayo
yamekanusha vikali za serikali hizo mbili.
No comments:
Post a Comment