Naibu mkuu wa polisi bandia afikishwa mahakamani

Afisa halisi wa polisi nchini Kenya wakati wa machafuko ya kisiasa

Mtu mmoja amefunguliwa mashtaka nchini Kenya ya kuwalaghai watu kuwa yeye ni naibu kamishna wa polisi kwa kipindi cha miaka mitano.

Joshua Waiganjo amesemekana kuwafuta kazi na kuwaajiri maafisa wengine wa polisi katika mkoa wa Rift Valley wakati huo.

Mshukiwa huyo alikanusha madai ya kujifanya kuwa afisa wa polisi, kumiliki mavazi ya polisi na pia kuwaibia watu kwa nguvu.

Mshukiwa huyo inasemekana aligunduliwa baada ya kusafiri kwa ndege ya polosi kwenda kuchunguzi mauaji wa maafisa wa polisi.

Mwezi Novemba, takriban maafia 42, wa polisi waliuawa na wezi wa mifugo, katika bonde la Suguta, shambulio ambalo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya taifa hilo.

Baada ya kukana mashtaka hayo, kesi hiyo ilihairishwa ili kumruhusu mshukiwa huyo kutafuta matibabu kutokana na ugonjwa wa kisukari katika hospitali moja nchini humo.

No comments:

Post a Comment