WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe
amekutana na malalamiko mazito kutoka kwa Chama cha Wakala wa Forodha
(TAFFA) ambao wamedai kuna wamiliki wa meli ambao pia wanafanya kazi ya
kuingiza na kutoa mizigo bandarini jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Kwa
mujibu wa sheria za Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri wa Majini
na Nchi Kavu (Sumatra) ni marufuku kampuni ya wakala wa meli kuwa na
leseni ya kuingiza na kupakuwa mizigo bandarini.
Akizungumza mbele ya Waziri Mwakyembe ambaye
alialikwa katika mkutano uliohusisha wadau wa kampuni za ushuru wa
forodha, Makamu mwenyekiti mstaafu wa Taifa, Otieno Igogo alisema,
Serikali imekosa macho ya kuona baadhi ya udanganyifu unaotumiwa na
baadhi ya vigogo kupitia mamlaka za hapa nchini.
Waziri Mwakyembe alidai kushtushwa na tuhuma
hizo na aliagiza apewe majina ya kampuni hizo haraka ili aweze kuchukua
hatua dhidi yao.
“Hatuwezi kuonekana kama tuko likizo lazima mniletee ushahidi ofisini kwangu,” alisema.
kiongozi
huyo mstaafu Taifa. Alibainisha katika mkutano huo kuwa , kitendo cha
umiliki wa leseni mbili kwa kampuni hizo kunaweza kuruhusu mazingira
yanayoshawishi vitendo vya kifisadi kufanyika kwa urahisi.
“Kampuni ya kupakuwa mizigo halafu pia
inahusika na uwakala wa kupokea mizigo ya nje ya nchi na kutoa ndani ya
nchi, Mheshiwa Waziri tunaomba uangalie hilo kwani pia linaondoa
ushindani wa kibiashara,”alisema Igogo.
Alizitaja baadhi ya kampuni hizo kuwa ni
pamoja na Swizz Port na DHL huku akiitupia lawama mamlaka ya Sumatra kwa
kushindwa kuzichukulia hatua kampuni hizo.
Igogo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Walipa
Kodi nchini aliongeza kuwa kwa mujibu wa sheria katika umiliki wa
kampuni za uwakala wa meli,Mtanzania anatakiwa kuwa na asilimia 51 ya
umiliki lakini mpaka sasa hakuna kampuni hata moja inayomiliki
asilimia hizo.
“Mheshimiwa Waziri, Kampuni hizo wanamiliki kampuni za meli, Watanzania wameshikizwa kama kivuli tu”alisema Igogo.
No comments:
Post a Comment