JESHI la
polisi limekumbwa na
kashfa nyingine baada ya askari wake
kudaiwa
kumpiga risasi msichana wa
miaka 16 baada ya kumkuta akivunja amri ya
sita ndani ya gari.
(Jina
tunalihifadhi) alikumbana na mkasa huo
Jumatano usiku eneo la Mbagala
Zakhem
jijini Dar es Salaam, ambapo alipigwa
risasi sehemu ya makalio
wakati
akijaribu kuwakimbia polisi kwa
kutumia gari la mpenzi wake.
Mpenzi huyo (jina linahifadhiwa),
alikamatwa na kuwekwa mahabusu na
kufunguliwa kesi ya ubakaji.
Akizungumza
na NIPASHE Jumapili jana katika wodi
ya Hospitali ya Temeke alikolazwa,
msichana
huyo alisema siku ya tukio alikutana na
kijana huyo majira ya
saa 8:00 usiku
katika baa moja inayoitwa Kindau na
kukubaliana kwenda
kushiriki
tendo la ndoa kwa malipo ya Sh 20,000.
Alisema kutokana na
muda huo kuwa
usiku sana hawakuweza kwenda katika
nyumba ya kulala
wageni na badala yake
walikwenda eneo la Zakhem na kisha
walipaki gari
kwenye uchochoro na
baadae walianza kubanjua amri ya sita.
Wakiwa kwenye kilele cha mapenzi yao
, ghafla walishtukia gari la polisi likiwajia
kwa kasi kwa nia ya kuwakamata.
“Tuliagana
anilipe elfu ishirini wala
hakunibaka kama anavyodai, wao
polisi
walitukuta tayari tunamaliza
lakini kutokana na woga
tulikimbia ili
tusikamatwe,” alisema msichana huyo.
Alisema
wakati wanakimbia
kwa kutumia gari la mpenzi wake
askari mmoja alifyatua
risasi
iliyopenya kwenye taa ya gari na
kwenda kumjeruhi sehemu ya
makalio yake.
“Nilisikia mlio mkubwa wa bunduki,
ghafla nilihisi kitu kimeingia mwilini
mwangu na kuishiwa nguvu,” alisema kwa uchungu.
Alisema
kwa kuona hali hiyo,
mpenzi wake alisimamisha gari kwa
kujisalimisha na
polisi walipowafikia
walimtaka mpenzi wake huyo atoe pesa
kama malipo ya
kitendo chao cha
kukutwa wakifanya mapenzi
ama sivyo watampeleka
kituoni.
Alieleza
kuwa mpenzi wake hakuweza
kutoa pesa hizo ndipo walipoamua
kumpiga na
kumpeleka kituo cha
polisi cha Mbagala na yeye alifikishwa
hospitalini
hapo kwa ajili ya matibabu.
Hata
hivyo, ndugu na jamaa wa mpenzi
wake wanapinga hatua ya polisi hao
kutumia nguvu kubwa kama watu hao
walikuwa watuhumiwa wa ujambazi.
Wakizungumza
wakiwa kwenye kituo
cha Polisi cha Mbagala kufuatilia
hatma ya ndugu
yao, ndugu hao
ambao hawakutaka majina yao
yatajwe gazetini walisema
hatua ya
polisi kupiga risasi huku wakitambua
watu hao sio majambazi ni
kitendo cha kinyama.
“Tunachoshangaa
ni kwa nini polisi
wapige risasi wakati wakijua hawakuwa
majambazi ila
walikuwa wakifanya
mapenzi, hata hilo jalada la kesi
walilofungua
wanataka kuficha maovu
yao na sio vinginevyo,” alisema ndugu
mmoja
ambaye alijitambulisha kuwa shemeji yake.
Alisema
kimsingi tukio hilo lilikwenda
katika makubaliano yao na sio ubakaji
kama wanavyodai, ila kinachofanyika
kwa sasa ni kutaka kumlinda askari
mwenzao aliyejeruhi kwa risasi.
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke,
David Misime, alipopigiwa simu kuelezea
tukio hilo, alisema kwa sasa hawezi
kulizungumza kwa kuwa yupo nje ya
Mkoa kikazi.
No comments:
Post a Comment