Wananchi wavunja mkutano Wakimkataa Mwenyekiti

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Robert Kitimbo akiwaelekeza jambo maafisa wa polisi walopokuwa kwenye Mkutano wa Hadhara ulioitishwa na wananchi wa kitongoji cha Njedengwa hata hivyo mkutano huo ulivunjika ktokana na wannchi kumkataa Mwenyekiti wao Denis Said.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Robert Kitimbo Akijadiliana jambo na polisi waliofika katika mkutano wa Hadhara uliovunjika kwa shinikizo la wananchi waliokuwa wakimkataa Mwenyekiti wa kitongoji chao Njedengwa Denis Said aliyekaa mwisho kushoto na anaemfuatia ni Mwenyekiti wa kijiji Cha Dodoma Makulu Bedson Chidumule.

Wananchi wa Kitongoji Cha Njedengwa Kata ya Dodoma Makulu Wakiwa na Mabango yenye Ujumbe wa kumkataa Mwenyekiti walipokuwa kwenye Mkutano wa Hadhara walioudai wananchi hao ambao hata hivyo ulivunjika kutokana na wananchi hao kugoma Mwenyekiti huyo Denis Said asifungue mkutano.


Mmoja wa Wakazi wa Kitongoji Cha Njengwa Khatib Mayuni akionyesha Ramani Ya ujenzi wa nyumba za kitongoji hicho waliyoikamata kwa watu waliojitamburisha kuwa ni wafanya kazi wa CDA ambao walipoombwa vitamburisho wakatimua mbio huku uongozi wa eneo hilo ukiwa haujui lolote


John Banda,DODOMA

Mkutano  mkuu wa wakazi wa Kitongoji cha Njedengwa Chini ya mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Robert Kitimbo na Afsa Utumishi Lawrence Malangwa ulivunjika jana kutokana na baadhi ya wakazi hao kumkataa mwenyekiti wa Kitongoji hicho Denis Said asifungue mkutano huo kwa madai kuwa hawamtambui.

Kitongoji hicho kiko katika kata ya Dodoma Makulu, Manispaa ya Dodoma na kwamba kimekuwa katika migogoro ya mara kwa mara ambapo mkuatano kama huo ulioitioshwa na wananchi hao na kuhudhururiwa na Meya mwanzoni mwa mwaka huu uliwahi kuvunjika kwa sababu kama hiyo.

Mkurugenzi wa huyo aliwasili katika mkutano huo ambao ulikuwa umeandaliwa na wakazi wa Kitongoji hicho kwa madai kuwa Mwenyekiti wa kitongoji hicho ameshindwa kuitisha mikutano ya kitongoji  kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.

Alipofika katika mkutano huo Kitimbo alimkaribisha mwenyekiti huyo ili afungue mkutano, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida  wananchi  hao walipaza sauti zao kuwa hawataki mwenyekiti huyo afungue mkutano kwa madai kuwa hawamtambui.

Ili kuokoa jahazi Mkurugenzi huyo alijaribu kuwatuliza wananchi ili wakubali mwenyekiti huyo afungue mkutano na kama kuna mambo mengine watayazungumza baadaye baada ya mwenyekiti huyo kufungua mkutano.

Lakini hata hivyo juhudi zake hazikuzaa matunda kwani kulizuka zogo kubwa la watu kumkataa mwenyekiti huyo na kudai ni afadhari ateuliwe mwingine wa muda afungue mkutano, hali iliyomfanya Mkurugenzi kuita polisi eneo la tukio ili kuja kutuliza ghasia ambazo zingeweza kujitokeza.

Hata baada ya polisi kuwasili katika eneo hilo wakazi hao waliendelea na msimamo wao huo wa kumkataa mwenyekiti huyo na kusababisha kutokuwepo kwa maelewano baina yao.

Baada ya Kitimbo kuona kuwa hali si shwari katika eneo hilo aliamua kuondoka na ujumbe wake waliokuwa wamefika kwenye mkutano huo kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuwaacha wananchi wa kitongoji hicho wakiwa wamegawanyika katika makundi mawili.

Kundi la kwanza ni lile lililokuwa likimkataa mwenyekiti na kutaka wachague mwenyekiti wa muda ili awafungulie mkutano wao na kundi la pili ni lile lililokuwa likimtaka mwenyekiti huyo afungue mkutano ili waweze kuwasilisha kero  zinazowakabili.

Hata hivyo ilionekana kuwa kundi la kumpinga mwenyekiti huyo lilikuwa na nguvu na kwamba lilikuwa limejipanga vizuri kwani lilisababisha mkutano huo kuvunjika na haijulikani utaitishwa lini tena na nani atausimamia wakati Mkurugenzi alishindwa.

Katika madai yao ya msingi wakazi hao walikuwa wanamtuhumu mwenyekiti huyo kutoitisha mikutano mikuu ya kitongoji hicho kwa ajili ya kuwasomea mapato na matumizi ya kitongoji hicho kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo pamoja na ubadhirifu wa mali ya Kitongoji.

Aidha baadhi ya wananchi walisikika wakidai kuwa Mkurugunzi ameshindwa kusimamia matakwa ya wananchi maana wao ndiyo waliomchagua Mwenyekiti huyo na wao ndiyo hawamtaki kwanini katumia hasira badala ya kuamua kidemokrasia yaani kwa kusema wengi wape.

‘’Mkurugenzi ameshindwa kusimamia matakwa yetu kama wakazi husika sisi ndiyo tunajua matatizo yetu na jinsi mwenyekiti asivyotusaidia, tutaenda mbele zaidi ikiwomo Bungeni maana kama ulivyoona Mkurugenzi kambeba Mwenyekiti wake’’, alisema Khatib Mayuni.


Mwisho.

No comments:

Post a Comment