Mbunge wa Viti Maalumu Mariam Msabaha (Chadema)
amesema, kitendo ha baadhi ya askari kukaa uraiani kinasababisha askari
hao kujiingiza katika masuala ya uhalifu.
Msabaha alitoa kauli hiyo alipouliza swali la
nyongeza bungeni, ambapo alihoji kuwa hali hiyo ya askari kuishi uraiani
ni kutokana na upungufu wa nyumba za askari unaosababishwa na Serikali
kutotoa kipaumbele kwa kada hiyo.
“ Je, Serikali inasema nini katika kuhakikisha
nyumba za askari zinajengwa nchi nzima ili watumishi hao wakae kambini
na kujiepusha na kujiingiza kwenye masuala ya uhalifu?” alihoji Msabaha.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima
alisema polisi wawapo chuoni wanafundishwa mambo yote isipokuwa
yanayotokea wawapo kazini ni makosa ya kibinadamu ambayo wizara hiyo
inayafanyia kazi.
Alisema Serikali kupitia polisi, haioni haja ya kuongeza muda au mitalaa ya mafunzo ya awali kwani muda unatosha.
kuwapatia ujuzi na weledi wa kutosha.
Kuhusu ujenzi wa nyumba za askari nchini, alisema
tatizo hilo limekuwa kubwa kutokana na kutochukuliwa hatua mapema lakini
hivi sasa linashughulikiwa.
Kiongozi huyo alisema Serikali ina mpango wa
kuboresha makazi ya askari kwa kukarabati na kujenga nyumba mpya ili
wote waishi kambini, lakini akabainisha kuwa ufinyu wa bajeti
unachangia.
No comments:
Post a Comment