Huu ni mchango wa Profesa Joseph Mbelea, anasema...
"Ingekuwa
bora kama hao wangekuwa maktabani kuliko kupoteza muda wao kwenye
kijiwe hiki cha abracadabra. Wangetumia muda wao maktabani wakisoma
vitabu na majarida wangekuwa wanajiongezea ujuzi, maarifa, na elimu kwa
ujumla. Sio tu ni jambo la manufaa kwa mtu kuelimika, bali pia
maandalizi ya ajira.
Kwa mfano, wangetumia muda wao maktaba na kusoma vitabu vya
ki-Ingereza, hatimaye wangekuwa na uwezo wa kushindana na wa-Kenya
kwenye ajira katika sekta kama utalii. Sekta hii inavyokwenda ni kwamba
hata mfagiaji anatakiwa kujua ki-Ingereza kidodo, ili mtalii akiomba
shuka au sabuni, aweze kujibiwa.
Lakini hao wa-Tanzania ukiwauliza habari hii ya ajira, wengine
watakuambia wanangoja ajira milioni walizoahidiwa na CCM mwaka 2012.
Wengine watakuambia serikali ya JK imeshindwa kuwapa ajira. Na kuna
siku mhubiri atakuja eneo hili hili na kuwahubiria kuwa wamekosa ajira
sababu ya mfumo Kristo. Tena hii abracadabra ya mfumo Kristo imepamba
moto kweli.
Inabidi sisi wenye ufahamu wa dunia, kutokana na kutembea sehemu mbali
mbali za dunia, na pia kutokana na kusoma, tufanye juhudi ya kuwamegea
hao wenzetu elimu ambayo Mungu katupa fursa ya kuipata. Kwa upande
wangu, naandika sana kwenye blogu, makala, na hata vitabuni, kuwa dunia
ya leo haina mchezo, na njia pekee ya kuimudu na kujipatia mafanikio
ni kwa kujielimisha. Ndugu zetu waache kushabikia hizo abracadabra, na
badala yake wasome vitabu au kwenda shuleni, kwani. Nyerere alisema
elimu haina mwisho, na ndilo fundisho la kuzingatiwa."
No comments:
Post a Comment