|
Abdallah Juma wa Simba SC, mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kucheza Ligi Kuu |
Na Prince Akbar
MICHUANO
ya Ligi Kuu kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kwa msimu wa 2012/2013
itaanza Septemba 15 mwaka huu kwa timu zote 14 kujitupa kwenye viwanja
tofauti.
Mechi
za ufunguzi zitakuwa kati ya Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam), Polisi Morogoro vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro),
Tanzania Prisons vs Yanga (Sokoine, Mbeya), Mgambo JKT vs Coastal Union
(Mkwakwani, Tanga), JKT Ruvu vs Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es
Salaam), Kagera Sugar vs Azam (Kaitaba, Bukoba) na Toto Africans vs
Oljoro JKT (Kirumba, Mwanza).
Mzunguko
wa kwanza (first round) utamalizika Novemba 11 mwaka huu ambapo kwenye
mzunguko huo mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itachezwa Oktoba 3
mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi
hiyo itamalizika Mei 18 mwakani kwa mechi kati ya Toto Africans vs Ruvu
Shooting (Kirumba), Mgambo JKT vs African Lyon (Mkwakwani), JKT Ruvu vs
Mtibwa Sugar (Azam Complex), Tanzania Prisons vs Kagera Sugar
(Sokoine), Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Azam (Sheikh
Amri Abeid Kaluta) na Polisi Morogoro vs Coastal Union (Jamhuri).
Endapo
Simba na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi
ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa
marekebisho.
Wakati
huo huo: Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi
rasmi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 kati ya bingwa
mtetezi Simba na makamu bingwa Azam itachezwa Septemba 11 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment