Mtoto
aliyepigwa na askari polisi hadi kupoteza fahamu,Kadogoo
Kalanga(16)mkazi wa Orkesmet Wilayani Simanjiro akiwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi(ICU) ndani ya hospitali ya Selian akiwa anahudumiwa
na manesi hospitalini hapo juzi jijini Arusha
-
WAMSHAMBULIA KWA MARUNGU NA KUMBANA SEHEMU ZAKE ZA SIRI HADI KUTOKWA NA HAJA NDOGO.
-
APOTEZA FAHAMU NA KULAZWA WODI YA WAGONJWA MAHUTUTI.
JESHI
la Polisi Mkoani Manyara limeingia katika shutuma nzito baada ya
Askari wake wa tatu kutuhumiwa kumpiga mtoto mwenye umri wa miaka 16
wa jamii ya kifugaji anayejulikana kwa jina la Kadogoo Kalanga mkazi wa
Orkesmet Wilayani Simanjiro hadi kupoteza fahamu.
Tukio
hilo lilitokea Jumatatu Agosti 28, 2012 majira ya saa tano na nusu
katika eneo la Orkesmet ambapo askari watatu mmoja wao akitambulika kwa
jina moja tu la John walimkamata mtoto huyo mara baada ya kumtuhumu
kuiba mbuzi wa jirani yake ambaye anajulikana kama Mama Shedi mkazi wa
eneo hilo la Orkesmet.
|
Mmoja
wa ndugu wa kijana huyo akiwa anawaonyesha waandishi wa habari ambao
hawapo pichani nguo(kaptula) ya kijana aliyepigwa na askari polisi
hadi kupoteza fahamu namna ilivyokuwa imechanika chanika baada
kushushiwa kipigo
|
Mashuhuda
wanadai kuwa polisi hao baada ya kumkamata mtoto huyo, walianza
kumuadhibu bila huruma hali iliyopelekea mtoto huyo kulazwa katika wodi
ya wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Selian iliyopo jijini
Arusha.
Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa hakuna jarida lolote lililofunguliwa
kutokana na kisa hiki. Watu wakaribu na mtoto huyu wanadai kuwa
walitaka kufungua mashtaka dhidi ya askari waliofanya unyama huo
lakini walikataliwa.
MAMA
MZAZI WA KIJANA KADOGOO KALANGA AMBAYE ALIPIGWA NA MAASKARI WA KITUO
CHA OLKESIMETI AKIWA ANAONYESHA SEHEMU AMBAZO MTOTO WAKE ANAMAUMIVU
MAKALI BAADA YA KUPIGWA
Akizungumza
na waandishi wa habari nje ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
ndani ya Hospitali ya Selian mama mzazi wa kijana huyo, Bi. Paulina
Kalanga alisema kwamba askari hao watatu walimfuata kijana wake eneo
la mnadani na kumtuhumu kuiba mbuzi na kuanza kumshumbulia kwa kumpiga
bila kumpa nafasi ya kujitetea kitendo kilichopelekea kuanza kutokwa
na haja ndogo mfululizo na kisha kupoteza fahamu.
“Yaani
walimkamata kijana wangu kisha wakaanza kumpiga kwa marungu na mateke
….. wakazishika sehemu zake za siri na kuanza kugongagonga na kitako
cha silaha ya moto ndipo alipoanza kujikojolea mfululizo na kupoteza
fahamu”alisema huku machozi yakimtiririka
WAFANYAKAZI
WA HOSPITALI YA SELIANI WAKIWA WANAMUHAMISHA HOSPITALI MTOTO HUYO
BAADA YAKUKOSA KIFAA CHA KUMPIMIA KATIKA HOSPITALI HIYO NA KUMPELEKA
HOSPITALI YA AGAKAN
Taarifa
zinasema kuwa polisi hao baada ya kuona hali ya mtoto huyo imekuwa
mbaya walimbeba na kisha kumkimkimbiza haraka katika kituo cha afya cha
Orkesmet kwa ajili ya matibabu kabla ya wanandugu kuomba gari la
wagonjwa mahututi (ambulance) kumkimbiza katika hospitali ya Selian
iliyopo mkoani Arusha.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoani Manyara, Akili Mpwapwa alipohojiwa juu ya
tukio hilo alikiri kupata taarifa zake huku akisema kwa kifupi kwamba
tayari ameshatoa maelekezo kwa mkuu wa polisi wilayani humo kufanya
uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na kisha aletewe ripoti kamili
mezani kwake.
“Nimeshatoa
maelekezo kwa OCD kwamba uchunguzi wa kina ufanyike na nipewe ripoti
kamili kwa kuwa jana ndiyo nilipigiwa simu na kuelezwa juu ya tukio
hilo”alisema
Hatahivyo,aliongeza
kwa kusema kwamba endapo kuna askari atabainika kuhusika na tukio
hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
“Ikibainika askari amehusika basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa na hapa tayari uchuinguzi unaendelea”alisema
No comments:
Post a Comment