CHAMA
cha Viziwi Tanzania Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kimeitaka
Halmashauri ya wilaya hiyo kutoa fedha zinazotengwa na serikali kwa
ajili ya mfuko wa walemavu wa Ukimwi.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa mradi wa mafunzo yalugha ya alama
Wilaya Kondoa Mustaph Shabani, kwenye mafunzo ya lugha ya alama
yaliyofadhiliwana shirika la The Foundation for Civic Society (FCS)
kwa ajili ya watumishi wataasisi mbalimbali za kiserikali iliyofanyika Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma.
Shabani amesema chama cha viziwi kinashangazwa kuona Halmashauri hiyo
ikishindwa kuwapatia fedha hizo ambazo zimekuwazikitengwa na serikali
kila mwaka kwa ajili ya maendeleo ya walemavu.
Amesema Chavita inatambua serikali kwa kupitia Halmashauri zake hapa
nchini imekuwa zikitenga fungu hilo kwa ajiliwalemavu lakini Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kondoa Dorosta Katokwa upande wake aliwataka
watumishi wa idara ya Afisa Maendeleo na Jamii naAfisa
Maendeleo ya Jamii walifikishe suala hilo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kama kuna fungu hilo kwa ajili ya jamii wasiojiweza.
Dorosta amesema fungu hilo kama lipo kwa Mkurugenzi nihaki yao hivyo
hakuna sababu ya kutolifuatilia wakati viziwi hao wanamahitajimengi
wanayokabiliana nayo yakiwemo ya ugonjwa wa ukimwi.
Kwea upande wao wazazi na Walezi wa watoto wenye ulemavu wa kutosikia
(viziwi) wameomba mradi wa mafunzo ya lugha ya alama unaofadhiriwa na
shirikalisilo la kiserikali la the Foundation for Civic Society,
kuwapatia mafunzoya muda mrefu yatakayo warahisishia uwelewa zaidi wa
elimu ya mawasiliano pindiwanapokuwa na
familia zao.
Mmoja wa wazazi haoFatuma Raffa alisema wametoa ombi hilo kutokana na
muda unaotolewa wa mafunzo ya lugha ya alama kuwa mdogo kwa kuwa wazazi
walio wengi hawana elimuya uwelewa wa mawasiliano
No comments:
Post a Comment