Raia wakijaribu kuwaokoa watu kufuatia shambulio la kigaidi mjini Nairobi
Wakimbizi wote wenye asili ya
Kisomali nchini Kenya, wameamriwa kuondoka katika maeneo ya mijini na
kurudi kambini baada kuwepo kwa milipuko ya mara kwa mara.
Misaada haitatolewa tena kwa yeyote ambaye atakuwa mjini, amesema mkuu wa shirika la wakimbizi la umoja wa mataifa.
Milipuko hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara
katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu wenye asili ya Kisomali, kama
vile mkoa wa Kaskazini Mashariki na mtaa wa Eastleigh iliyoko mjini
Nairobi.
Mashambulizi hayo yanaaminika kufanywa na watu wanaoaminika kuwa wanachama cha kundi la Kiislamu la Al Shabab.
No comments:
Post a Comment