Libya bado haijakombolewa kikamilifu
Kiongozi wa mpito wa Libya,
Mohammed Magarief, amesema kuwa mwaka mmoja baada ya Kanali Gaddafi
kuuwawa, nchi bado haijakombolewa kikamilifu.
Bwana Magarief - ambaye anaongoza bunge - alitoa
mfano wa hali katika mji wa Bani Walid, shina la Gaddafi, ambako hivi
karibuni kumetokea mapambano baina ya wapiganaji wanaounga mkono
serikali na wale wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Gaddafi.
Bwana Magarief piya alisema kuchelewa kufanya
mabadiliko ya idara ya sheria na kuunda jeshi na kikosi cha polisi
rasmi, pamoja na kushindwa kuwanyang'anya silaha wapiganaji, kunazidisha
wasiwasi.
No comments:
Post a Comment