Idadi ya meli zinazotekwa na
maharamia katika pwani ya Somalia, zimepungua sana mwaka huu , kulingana
na shirika la kimataifa la safari za majini.
Ni meli sabini pekee zilitekwa nyara katika
miezi ya kwanza tisa mwaka huu ikilinganishwa na visa 233
vilivyoripotiwa mwaka 2011.
Juhuzi za kimataifa pamoja na
mikakati kipya ya kiusalama ndiyo imekuwa changamoto kubwa kwa maharamia
kuendesha kazi zao kulingana na shirika hilo.
Lakini shirika hilo limetoa tahadhari kwa mabaharia kuwa makini wakati wa shughuli zao hasa katika pwani ya Somalia
Mkurugenzi wa shirika hilo, Kapteni Pottengal
Mukundan, alisema ni habari njema kusikia kuwa uharamia umepungua,
lakini mabaharia hawapaswi kulegea katika kuchukua tahadhari.
Uharamia umeripotiwa zaidi katika Ghuba ya
Guinea, ambako jeshi la wanamaji la Nigeria limeanza kushika doria.
Pwani mwa Benin na Togo pia ni hatari.
Shirika hilo linasema kuwa visa vya utekaji
meli, hupangwa kwa lengo la kuiba mafuta ambayo yanaweza kuuzwa bila
wasiwasi katika masoko ya nyumbani.
Ingawa ni kisa kimoja tu kimeripotiwa nchini
Somalia katika miezi mitatu iliyopita , maharamia wangali wanazuilia
meli kumi na moja wakidai kikombozi huku wafanyakazi 167 wa meli hizo
pia wakiwa wamekamatwa.
Wafanyakazi wengine 21 wanazuiliwa katika nchi kavu, wengine sasa wamekuwa wakizuiliwa kwa zaidi ya miezi thelathini.
No comments:
Post a Comment