Mahakama za Gacaca zilisika baadi ya kesi za mauaji ya kimbari nchini Rwanda
Mahakama ya
Norway imeanza kusikiliza mashahidi katika kesi dhidi ya Bwana Sadi
Bugingo, raia wa Rwanda anayeshtakiwa kwa makosa ya mauaji ya kimbari ya
mwaka 1994.
Mashahidi wanasikilizwa na mahakama hiyo wakiwa mjini Kigali kwa kutumia teknolojia ya video.
Hii ni kesi ya kwanza ya mauaji ya kimbari ya Rwanda kusikilizwa na nchi ya Norway.
Mwandishi wa BBC mjini Kigali Yves Buchana,
anasema kuwa mashahidi 3 wamesikilizwa na mahakama hiyo ya mjini Oslo
wakiwa katika chumba cha mahakama nchini Rwanda.
Mashahidi wawili waliotangulia walikuwa wa
upande wa utetezi wa Bwana Sadi Bugingo.Wote wamesikika wakisema kuwa
wanamfahamu kama mfanyabiashara aliyekuwa anasaidia watu wala
hawamfahamu katika vitendo vya uhalifu.
shahidi wa pili mwanamke kutoka kabila la
watutsi ambaye amesema ni shemeji wa mtuhumiwa huyo amesema kuwa wakati
wa mauaji ya kimbari Sadi Bugingo aliwahi kuwasaidia walipovamiwa na
kundi la wanamgambo likitaka kuwaua akafanikiwa kulishawishi lisiwauwe.
Jumla ya mashahidi 70 wanatarajiwa kusikilizwa
baadi wakiwa wa upande wa utetezi wengine wakiwa dhidi ya
mshukiwa.Buchana anasema kuwa mashahidi wanaulizwa maswali na upande wa
mashtaka na upande wa utetezi kwa kutumia teknolojia ya video.
Sadi Bugingo mwenye umri wa miaka 47 alikuwa
mfanyabiashara na mwenye ushawishi mkubwa katika wilaya ya Ngoma mkoa wa
mashariki ambako inadaiwa alifanyia makosa wakati wa mauaji ya kimbari.
Rwanda inamtuhumu kuhusika na mauaji ya
kimbari,uhalifu wa kivita kuhamasisha mauaji hayo na kuunda genge la
wahalifu.Hii ni kesi ya kwanza kusikilizwa ya mauaji ya kimbari ya
Rwanda na mahakama ya Norway ,hatua ambayo imepongezwa na Rwanda licha
ya kwamba serikali ilikuwa imeomba kukabidhiwa mtuhumiwa huyo.
No comments:
Post a Comment