Wapiganaji wa kiisilamu walioteka Kaskazini mwa Mali
Wapiganaji wa kiisilamu wameuteka mji uliokuwa unadhibitiwa na wanajeshi wa serikali licha ya harakati za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao kwa usaidizi wa Ufaransa.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian alisema kuwa mji wa Diabaly, ambao uko umbali wa kilomita 400 kutoka mji mkuu ulitekwa katika makabiliano yaliyofanyika kati ya wapiganaji hao na wanjeshi Jumatatu.
Bwana Le Drian alisisitiza kuwa harakati za jeshi la Ufaransa zimeweza kupiga hatua.
Aliongeza kuwa wapiganaji hao waliweza kutoroka na kukimbilia Mashariki mwa nchi lakini akakiri kuwa wanjeshi wa Ufaransa wanakumbwa na wakti mgumu kukabiliana na waasi ambao ambao wamejihami vilivyo.
Awali waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius alisema kuwa harakati za jeshi la Ufaransa katika kusaidia wanajeshi wa Mali dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu hazitachukua muda mrefu sana.
Juhudi zao zitadumu tu wiki chache.
Mnamo Jumapili, Jeshi la wanahewa la Ufaransa liliimarisha mashambulio yake dhidi ya wapiganaji hao hasa kwenye miji ya Gao na Kidal.
Wizara ya Ulinzi ya ufaransa inasema mashambulizi hayo yatakamilika katika muda wa wiki kadhaa.
Maeneo ambayo tayari yametwaliwa na jeshi la Mali kwa usaidizi wa Ufaransa
No comments:
Post a Comment