WILAYA YA MOMBA MBEYA– MAUAJI
MNAMO TAREHE 13.01.2013 MAJIRA YA SAA
12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KALUNGU KIJIJI CHA IVUNA TARAFA YA KAMSAMBA
WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA.
WATU WAWILI AMBAO NI 1.ERNEST S/O
TWINI MOLELA NA MIZINARA D/O MILILO @ MATELA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IVUNA
WALIUAWA KWA KUPIGWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KISHA KUWAZIKA KATIKA KABURI MOJA .
CHANZO NI TUHUMA ZA KISHIRIKINA BAADA
YA MAREHEMU HAO KUTUHUMIWA KUWA NI WACHAWI KWA KUMLOGA MAREHEMU NONGWA S/O
HUSSEIN MOLELA ALIYEFARIKI DUNIA TAREHE 12.01.2013 MAJIRA YA SA 16:00HRS BAADA
YA KUUGUA MUDA MREFU.
TUKIO HILO LILITOKEA WAKATI WA
MAZISHI YA MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA AMBAPO KUNDI LA WATU WASIOPUNGUA
KUMI WALIPANDISHA HASIRA NA KUWATUHUMU MAREHEMU HAO KUHUSIKA NA KIFO CHA NDUGU
YAO NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA HIVYO KUANZA KUWASHAMBULIA KWA KUTUMIA NGUMI,
FIMBO NA MAWE KISHA KUWATUMBUKIZA KATIKA KABURI ALILOKUWA AKIZIKWA MAREHEMU
NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA WAKIWA HAI NA KUWAZIKA WOTE WATATU KATIKA KABURI HILO
MOJA.
BAADA YA HAPO WATU HAO WALIKWENDA
NYUMBANI KWA ERNEST S/O TWINI MOLELA NA KUICHOMA MOTO NYUMBA YAKE. KUFUATIA
TUKIO HILO WATUHUMIWA WAWILI WALIOKUWA VINARA WA TUKIO HILO WAMEKAMATWA AMBAO
NI 1. VENA S/O ERNEST MOLELA [MTOTO WA MAREHEMU ERNEST S/O TWINI MOLELA], MIAKA
26, MUWANDA, MKULIMA NA 2. EMANUEL S/O CHRISTOPHA, MIAKA 16, MUWANDA MKULIMA
WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IVUNA. MAREHEMU WOTE WATATU NI NDUGU WA UKOO
MMOJA. TARATIBU ZA KUFUKUA KABURI ILI MIILI YA MAREHEMU IFANYIWE UCHUNGUZI
ZINAFANYWA.
AIDHA TARATIBU ZINAFANYWA ILI
WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAHESHIMU NA KUTII SHERIA
PASIPO KUSHURUTISHWA.
PIA ANAIASA JAMII KUACHANA NA IMANI
ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII IKIWA NI PAMOJA NA
KURUDISHA NYUMA MAENDELEO.
AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII/KIKUNDI
CHA WATU WENYE KERO/MALALAMIKO,USHAURI ,UJUMBE MAALUM KUTAFUTA NJIA ILIYO
HALALI KUFIKISHA KERO,MALALAMIKO,USHAURI ,UJUMBE WAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO
BADALA YA KUTUMIA VURUGU/FUJO NA KUSABABISHA MAUAJI.
No comments:
Post a Comment