Polisi na wataalamu
wa kuchunguza maiti wamepigwa na mshangao mkubwa baada ya kukosa kupata
chochote ndani ya makaburi ya siri yaliyogunduliwa katika eneo la Tana River.
Polisi walipewa amri ya kufukua makaburi
hayo hii leo katika kijiji cha Ozhi ambako mapigano kati ya jamii za
Orma na Pokomo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu miamoja na kuwaacha
maelfu bila makao.
Kwa mujibu wa naibu kamishna wa polisi eneo la Tana River, Anthony Kamitu, makaburi hayo yalikuwa na mitaro minne ishara kuwa watu walikuwa wamezikwa kwenye makaburi hayo.
Ingawa bwana Kamitu alisema kuwa hawakupata
miili yoyote licha ya kuwa kulikuwepo na harufu mbaya ishara kwamba
maiti waliokuwa ndani ya makaburi hayo waliondolewa.
Bwana Kamitu anasema kuna hofu kuwa wahalifu
kutoka jamii ya Pokomo waliitoa hiyo miili kwenye makaburi hayo huku
polisi wakisubiri kibali cha mahakama ili kuweza kuyafukua.
Polisi wamefahamisha BBC kuwa makaburi hayo
yalikuwa tu na mguu mmoja wa kushoto wa mtu na wanashuku kuwa maiti
waliokuwa ndani ya makaburi hayo waliondolewa na kupelekwa kwingineko.
Zaidi ya watu miamoja wamefariki katika mapigano
kati ya jamii hizi mbili ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa mwezi
mmoja ulipita.
Makabiliano kati ya jamii hizo mbili yalianza katikati ya mwezi jana na kusababisha mashambulizi ya kuvizia na ya kulipiza kisasi.
No comments:
Post a Comment