Watu wa Benghazi wataka amani
Maelfu ya Walibya wamefanya
mhadhara katika mji wa Benghazi, mashariki mwa Libya, kuunga mkono
demokrasi na kuwapinga wapiganaji wa Kiislamu.
Waandamanaji waliisihi serikali ya
Libya iyapige marufuku makundi ya wapiganaji ambao wamekataa kukabidhi
silaha zao tangu vita dhidi ya Kanali Gaddafi mwaka jana.
Waandamanaji wanataka serikali izidishe jeshi na polisi, na walimsifu balozi wa Marekani aliyeuliwa mjini humo juma lilopita.
Waliimba wakati wakiandamana kuelekea medani kuu ya Benghazi.
Muandamanaji mmoja, Faisla al-Naas, alieleza sababu zao:
"Sisi tunaandamana kupinga kundi lenye silaha ambalo halidhibitiwi na serikali.
Wapiganaji hawa wanafaa kujiunga na serikali ili watu wakae kwa salama.
Nchi yetu imekuwa na mtafaruku."
Maandamano mengine ya kuunga mkono wapiganaji yalikuwa madogo sana.
No comments:
Post a Comment