Abu Hamza awasili Marekani
Mhubiri wa Kiislamu mwenye
msimamo mkali, Abu Hamza, na watu wengine wane wanaoshukiwa kuwa
magaida, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumamosi nchini Marekani
baada ya kusafirishwa kutoka Uingereza.
Juhudi zao zilizogharimu fedha
nyingi, kupinga kupelekwa Marekani, zilimalizika Ijumaa mjini London
baada ya mahakama makuu kutupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na Bwana
Hamza.
Washukiwa hao watano walisafirishwa kwa ndege punde baadaye kuelekea Marekani.
Abu Hamza anakabili mashtaka kadha, pamoja na njama ya kuanzisha kituo cha mafunzo ya kijeshi katika jimbo la Oregon, Marekani.
Yeye na washukiwa wawili watafikishwa mahakama ya New York, na wawili wengine watafanyiwa kesi Connecticut.
No comments:
Post a Comment