Kamati Ya Bunge Ya Masuala Ya Ukimwi Yataka Ripoti ARV Bandia Kutinga Bungeni
NA: MAGRETH KINABO – MAELEZO
KAMATI
ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi imeishauri serikali kutoa
tamko la kuelezea ni hatua gani inaendelea kuchukua baada ya
kusimamisha kazi baadhi ya viongozi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD)
kufuatia kuwepo kwa dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi( ARV)
katika kikao cha Bunge kitakachoanza mwishoni mwezi huu.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Lediana Mng’ong’o
wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za Bunge
jijini Dares Salaam kuhusu kuwepo kwa dawa hizo.
“
Sisi tungependa kuishauri serikali kuendelea kufuatilia na hatua za
kisheria pale itakapobaini katika uchunguzi huo ili tatizo hili
lisiendelee kutokea,” alisema Lediana ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum
Iringa.
Aliongeza
kuwa wanaishauri Mamlaka cha Chakula na Dawa (TFDA) kuwa na
wawakilishi katika kanda mbalimbali ili kuweza kudhibiti tatizo la
kuwepo kwa dawa bandia.
Aidha
kamati hiyo imelaani kampuni ambayo imeingiza dawa feki na imetaka
hatua za kisheria zichukuliwe.
Kamati hiyo imewataka watu wanaotumia dawa hizo kutoziacha , bali
waendelee kuzitumia kwa kuwa dawa zote si feki na pia zipo za kutosha.
No comments:
Post a Comment