Kampuni ya Shell mahakamani Uholanzi
Eneo la Niger Delta lina barabara chache na vijiji vingi havina umeme wala maji safi
Waakilishi wa kampuni kubwa ya
mafuta ya Shell, wamefika mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya
kuchafua mazingira nchini Nigeria.
Wakulima wanne kutoka eneo lililo na utajiri
mkubwa wa mafuta la Niger Delta nchini Nigeria leo wameifikisha Kampuni
hiyo kubwa ya mafuta ya Shell katika mahakama ya kimataifa ya uholanzi
kujibu madai ya uchafuzi wa mzingira katika vijiji vinne nchini Nigeria.
Kesi hiyo ni moja kati kesi ambayo
imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na vyombo mbali mbali vya habari
duniani. Ikiwa wakulima hao watashinda kesi hiyo, huenda ikatoa nafasi
kwa maelfu ya watu wanaodai fidia kutoka kwa makampuni kama Shell.
Wakulima hao wanasema uvujaji wa mabomba ya mafuta yanayomilikiwa na kampuni hiyo yameharibu mashamba yao na biashara ya samaki.
Wa-Nigeria hao wakiungwa mkono na wanaharakati
wa mazingira kutoka Uholanzi wanataka Kampuni ya Shell ilazimishwe
kusafisha mazingira na kulipa fidia kwa hasara iliyotokea huko Niger
Delta.
Kesi hiyo imewasilishwa mahakamani na wakulima
wanne wa Nigeria kwa ushirikiano na shirika moja la kutetea mazingira la
nchini humo, Friends of the Earth.
Ni mara ya kwanza kwa kampuni kubwa ya Uholanzi
inashtakiwa katika mahakama ya kiraia nchini humo kuhusiana na uharibifu
uliotokea katika nchi ya kigeni.
Shell, inasisitiza kuwa haijaweza kusafisha eneo ambalo lilichafuka kutokana na shughuli zake nchini Nigeria.
Inasemekana kuwa nusu ya uvujaji wa mafuta katika eneo hilo umesababishwa na visa vya wizi.
Kesi hiyo inahusishwa na uvujaji wa mafuta uliotokea katika eneo la Ogoniland nchini Nigeria.
Wakulima wanasema kuwa mafuta yaliyovuja kutoka
kwa mabomba ya mafuta ya kampuni hiyo, yameathiri mapato yao, kwa
kuharibu mimea na mabwawa ya samaki.
Mmoja wa walioshtaki kampuni hiyo, Alfred Akpan,
aliambia BBC kuwa mafuta yaliyovuja yaliharibu vibaya mabwawa yake 47
ya samaki na anataka fidia.
No comments:
Post a Comment