Malema ahusishwa tena na ufisadi
Julius Malema
Mwanaharakati wa kisiasa nchini
Afrika Kusini, Julius Malema, ameelezea kughadhabishwa na ripoti kuhusu
madai ya ufisadi yanayohusisha kampuni anayoimiliki.
Alisema kuwa uchunguzi uliofanywa na mhifadhi wa
mali ya umma, Thuli Madonsela kuhusu kampuni yake kupewa zabuni na
serikali , ilimpata na hatia ya ufisadi bila yeye mwenyewe kuwepo.
Bi Madonsela alisema kuwa hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya kampuni hiyo.
Mwezi jana,bwana Malema alikanusha madai ya kujipatia pesa haramu ambazo zilihusishwa na kutolewa kwa zabuni za serikali.
Mwanasiasa huyo mwenye utata na ambaye
amefurushwa kutoka chama tawala, kwa kuchochea migawanyiko chamani,
alisema kuwa kesi hiyo imeshinikizwa kisiasa.
Katika ripoti yake, kuhusu kutolewa kwa zabuni
za serikali, Bi Madonsela alidokeza kuwa zabuni ya huduma na
usafirishaji wa bidhaa iliyotolewa na idara ya serikali ya barabara na
usafiri katika mkoa wa Limpopo, kwa kampuni ya uhandisi ya On-Point
Engineering, haikuwa halali.
Aliongeza kuwa Bbwana Malema na mshirika wake wa
kibiashara wanaomiliki kampuni hiyo, walijinufaisha kwa vitendo fisadi
vya kampuni yenyewe na idara ya usafiri ya serikali.
Ripoti ilisema kuwa kampuni hiyo ilishinda
zabuni ya dola milioni 51 mnamo mwaka 2009 licha ya kwamba ilikuwa
imeendesha shughuli zake tu kwa mwezi mmoja, haikuwa na wafanyakazi wala
mali au kupata faida yoyote.
No comments:
Post a Comment