Siku Ya Kupunguza Maafa
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAMKO LA WAZIRI MKUU KATIKA KUADHIMISHA
SIKU YA KIMATAIFA YA UPUNGUZAJI WA ATHARI ZA
MAAFA DUNIANI TAREHE 12 OKTOBA, 2012
Ndugu Wananchi, leo tarehe 12 Oktoba, 2012 ni Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji wa
Athari za Maafa (International Day for Disaster Reduction). Siku hii huadhimishwa
tarehe 13 Oktoba ya kila mwaka.
Hata hivyo, kwa mwaka huu Sekretariati ya Kupunguza Athari za Maafa ya Umoja
wa Mataifa, imeelekeza kuwa siku hii iadhimishwe leo siku ya Ijumaa Oktoba 12,
2012. Kama ilivyo kwa miaka yote tangu siku hiyo ilipoanzishwa katika miaka ya 1990,
Sekretarieti hiyo hutoa Kaulimbiu ya mwaka husika. Kaulimbiu ya mwaka huu inasema,
“WANAWAKE NA WASICHANA – NGUVU ISIYOONEKANA KATIKA KINGA DHIDI YA MAAFA”
(WOMEN AND GIRLS –THE INVISIBLE FORCE OF RESILIENCE).
Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji wa Athari za Maafa kwa mwaka huu imewalenga
Wanawake na Wasichana kwa lengo la kutambua na kukubali mchango unaotolewa
katika jamii na mamilioni ya Wanawake na Wasichana katika kukabili athari za maafa
na Mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuleta manufaa katika shughuli za maendeleo na
Ndugu Wananchi, mtakubaliana na mimi kwamba mafanikio makubwa yatokanayo
na nguvu za wanawake na wasischana hayatambuliwi kwenye shughuli za maafa na
katika kufanya maamuzi kutokana na kutokutambua mchango wao katika jamii. Kwa
kulitambua hili ndiyo maana ujumbe wa mwaka huu unasisitiza kutambua ushiriki wa
1
wanawake na wasichana katika kulinda na kujenga jamii kabla na baada ya Maafa.
Ndugu Wananchi, lengo kubwa la kaulimbiu ya mwaka huu ni kuamsha uelewa wa
wananchi katika masuala yafuatayo:-
i. Jamii kutambua mchango wa Wanawake na Wasichana kabla, wakati na baada
uwezo
wa
Wanawake
na
kutokushirikishwa katika shughuli za upunguzaji wa athari za maafa na katika
kutoa maamuzi kwenye ngazi za uongozi pamoja na mipango ya progamu na
uelewa mdogo wa jamii juu ya usawa wa jinsia;
iii.Kuondokana na mtazamo kwamba daima wanawake na wasichana ndiyo
waathirika wakubwa wa maafa; na
iv. Kudhihirisha vielelezo vya shughuli na jitihada zinazofanywa na Wanawake na
Wasichana katika kukabiliana na maafa.
Ndugu Wananchi, napenda nielezee hatua chache zilizochukuliwa na Serikali yetu
kuwezesha ushiriki wa wanawake katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa
ni pamoja na shughuli za upunguzaji athari za maafa katika ngazi za kisiasa na kutoa
maamuzi kwa kuwapa fursa ya moja kwa moja katika kusimamia Ofisi za Umma
zikiwamo Wizara, Taasisi na Idara pamoja na kutambua umuhimu wao katika uandaaji
wa sera, mikakati na mipango ya kiuchumi.
Ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi wa kisiasa mathalan, Wabunge
Wanawake wameongezeka kutoka asilimia 11 mwaka 1990 hadi kufikia asilimia 36
mwaka 2011. Kwa upande wa Mawaziri waliongezeka kutoka asilimia 12 mwaka 1990
hadi kufikia asilimia 27.5 mwaka 2011. Aidha, kwa mara ya kwanza mwaka 2010
katika historia ya nchi yetu aliteuliwa Mwanawake kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri
wa Muungano wa Tanzania. Kwa upande wa Wakuu wa Mikoa wameongezeka kutoka
asilimia 10 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 29 mwaka 2012 wakati Wakuu wa Wilaya
wameongezeka kutoka Asilimia 19 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 32 mwaka 2012.
2
Kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Menejimenti ya Maafa ya mwaka 2004, Wakuu wa
Mikoa na Wilaya ndiyo Wenyeviti wa Kamati za Maafa katika ngazi zao.
Katika ngazi ya uongozi wa kiutendaji, Majaji wanawake wameongezeka kutoka asilimia
6 mwaka 1990 hadi kufikia asilimia 35 mwaka 2011. Wakurungezi wa Halmashauri
wameongezeka pia kutoka asilimia 6 mwaka 1991 hadi kufikia asilimia 26 mwaka 2011.
Tukizingatia Sera yetu ya Taifa ya Menejimenti ya Maafa ya mwaka 2004, Wakurugenzi
hao ndiyo Makatibu wa Kamati za Maafa za Wilaya zao ambazo zina majukumu ya
kusimamia masuala ya maafa katika maeneo yao.
Ndugu Wananchi, ili kuamsha uelewa wa jamii kutambua na kukubali umuhimu wa
wanawake na wasichana katika kukabili na kupunguza athari za maafa na mabadiliko ya
tabia nchi, Serikali imewezesha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera na Mikakati
ya maendeleo. Lengo la hatua hii ni kufikia usawa wa jinsia kwa kuanzisha jumla ya
Madawati ya Jinsia 188 katika Wizara 26, Wakala za Serikali Saba, Sekretariati za Mikoa
21, Halmashauri 133 na Idara inayojitegemea moja.
Aidha, Serikali imewajengea uwezo wanawake kupitia mafunzo ya fani mbalimbali
yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Mafunzo kwa Wanawake Tanzania (TFTW).
wanawake 445 waliwezeshwa kupata mafunzo ya muda mrefu na mfupi katika fani za
sheria, uongozi na utawala, mipango, sayansi na teknolojia, ushauri nasaha, ujasiriamali
Vilevile, kwa kuzingatia kuwa wanawake walikuwa wameachwa nyuma kimaendeleo
ikilinganishwa na wanaume, serikali imefanikiwa kutekeleza hatua mbalimbali za
kuwawezesha wanawake kiuchumi. Hatua hizo ni pamoja na kuanzisha na kuendesha
Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake mnamo mwaka 1993 kwa lengo la kutoa mikopo
yenye masharti nafuu kwa wanawake kupitia Halmashauri za Wilaya. Hadi sasa kiasi
cha Shilingi 2,005,234,000/- kimekopeshwa kwa wanawake 40,105 katika Halmashauri
zote 134 nchini. Aidha, katika kuwajengea wanawake na wanaume uwezo, Benki ya
Wanawake Tanzania hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2011 ilitoa mafunzo ya ujasiriamali
3
kwa wateja wake kabla ya kuwapatia mikopo wajasiriamali 5,246 wakiwemo wanawake
4,358 na wanaume 888.
Ndugu Wananchi, Taarifa ya Dunia ya Tathmini ya Upunguzaji Athari za Maafa ya
Mwaka 2011 (Global Assessment Report on Disaster Risk Reduction (GAR) 2011),
inabainisha kuwa nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania zinakubaliana kuwa kukosekana
kwa utaalamu wa kuingiza masuala ya jinsia katika mipango ya maendeleo imekuwa
ni kikwazo kikubwa cha kinga dhidi ya maafa. Ripoti hii imeonesha kuwa asilimia 26 ya
nchi ikiwemo nchi yetu ndizo zilizotoa taarifa ya umuhimu wa kujikita katika masuala ya
jinsia kama chachu ya maendeleo.
Ndugu Wananchi, kuna vipengele vitatu katika kampeni hii ambavyo ningependa
Wizara, Taasisi na Idara za Serikali pamoja na Wadau wote wa Maendeleo kwa
kushirikiana na wananchi wavizingatie ili nguvu ya wanawake katika kinga dhidi ya
maafa ionekane. Vipengele hivi vinatokana na ujumbe muhimu wa Siku ya Kimataifa ya
Upunguzaji Athari za Maafa 2012 ambavyo ni:
i. Wanawake na Wasichana Wawezeshwe kwa Usalama wa Kesho
Wanawake na Wasichana wawezeshwe katika kuchangia kuleta maendeleo
endelevu kwa kupunguza athari za maafa, hususani katika utunzaji wa mazingira
na usimamizi wa mali asili, utawala na mipango ya matumizi ya ardhi na miji
pamoja mipango ya kiuchumi na kijamii ambayo ndiyo mihimili ya kinga ya
ii. Wananawake na Wasichana Nguvu Kuu ya Mabadiliko
Ili jitihada za upunguzaji wa athari za maafa ziweze kuleta matokeo mazuri ni
vyema jamii iwashirikishe Wanawake na Wasichana katika uandaaji na utekeleji
wa sera, mipango na mikakati ya kinga dhidi ya maafa.
Asilimia 52 ya watu Duniani ni Wanawake na Wasichana, kwa upande wa
Tanzania ni asilimia 51 ambao ni miongoni mwa waathirika wa maafa. Hapa
nchini inakadiriwa kwamba wanawake hasa wa Vijijini wanatoa Asilimia 80 ya
4
wafanyakazi katika kazi hasa za mashambani na hivyo kutoa Asilimia 60 ya
chakula kinachozalishwa.
Hivyo uzoefu, ujuzi na uelewa wao ni muhimu sana katika mikakati na shughuli
za Upunguzaji wa Athari za Maafa na kuhimili mabadiliko ya tabia nchi. Mchango
ya Wanawake na Wasichana utakuwa na matokeo mazuri iwapo watashirikishwa
katika hatua zote za menejimenti ya maafa.
iii. Jamii yenye Kinga Dhidi ya Maafa ni Jamii Inayojali Jinsia
• Kutokuwa na Usawa wa Jinsia ni Udhaifu – Kuimarisha Usawa wa
Jinsia ni Kuimarisha Kinga Dhidi ya Maafa
Kutokuwa na usawa wa jinsia unawaweka wanawake, watoto na jamii nzima
katika hatari pindi majanga ya asili yanapotokea. Kwa hali hiyo tujenge na
kuboresha kinga dhidi ya maafa kwa kutoa elimu kwa uwiano sawa wa jinsia.
• Itambulike Kuwa Uwiano Sawa wa Jinsia Unaanzishwa na Elimu
Wanawake na Watoto lazima washiriki katika kufahamu jinsi ya kujiandaa,
kukabili na kupunguza athari za maafa katika jamii. Hili litawezekana kwa
kuwaelimisha wavulana na wasichana katika rika zote. Wanaume na wavulana
wakihusika wataweza kuondoa vikwazo vinavyowazuia wanawake na wasichana
kushiriki katika mzingo mzima wa upunguzaji athari za maafa.
na
Wasichana
ni
Njia sahihi ya mawasiliano ni ile inayohusisha pande mbili kwa kushirikisha sauti
za Wanawake na Wanaume katika kujiandaa, kukabili na kupunguza athari za
maafa. Hivyo, jamii itaweza kuwa na uwezo wa kujikinga dhidi ya maafa na
kupata maendeleo endelevu.
Ndugu Wananchi, pamoja na mambo yote haya kama tutaongeza mkazo katika
kutambua mchango unaotolewa na Wanawake na Wasichana kwa kuwashirikisha katika
kuandaa na kutekeleza shughuli za Upunguzaji wa Athari za Maafa na kutoa maamuzi
kwenye ngazi za uongozi pamoja na mipango ya progamu, sera na mikakati tunaweza
5
kuiona nguvu ya wanawake katika kinga dhidi ya maafa. Natoa wito kwa Viongozi
wote katika Wizara, Idara, Taasisi zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za
Mikoa na Halmashauri ziendelee kuzingatia masuala ya jinsia katika Sera na Mikakati na
Mipango yao ya maendeleo kwa lengo la kufikia usawa wa jinsia ili nguvu ya Wanawake
na Wasichana katika kinga dhidi ya maafa ionekana dhahiri kwa jamii. Ikumbukwe
kuwa, jukumu la kupunguza athari za maafa ni la jinsia zote. Kila mmoja pale alipo
atimize wajibu wake.
ASANTENI SANA
Mhe. Mizengo P. Pinda (Mb)
WAZIRI MKUU
No comments:
Post a Comment