Mkataba Wa Ujenzi Daraja Kilombero
Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Mhandisi Patrick
Mfugale (kushoto) na Mtendaji Mkuu kutoka kampuni ya ujenzi ya China
Railway 15 Bureau group Corporation (CR15G) Zhang Tonggang
(kulia) wakiweka saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Kilombero lenye
urefu wa meta 384 na ujenzi wa barabara zake za miingilio za lami(
kilometa 9.142).na jenzi wake utagharimu shilingi bilioni 53.2 .Hafla
hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.na kushuhudiwa na Waziri wa
Ujenzi, Dkt, John Magufuli (mwenye miwani) na kulia kwake na katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Balozi Herbert Mrango.Pichani kutoka kushoto ni
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Tanroads , Bibi Hawa Mmanga,Mbunge wa
Mikumi- Abdul Salim Ameir na Mbunge kutoka Morogoro Kusini Innocent
Kalgeris
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale
(kulshoto) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya China
Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G) Bw, Zhang Tonggang (kulia)
wakibadilishana hati baada ya kuweka saini kwaajili ya ujenzi wa darala
la Kilombero mkoani Morogoro, Daraja hilo lenye urefu wa kilometa 384
litagharimu shilingi bilioni 53.2. .Ujenzi wa daraja hilo
utaziunganisha Wilaya za Mahenge na Ulanga. pamoja na kuboresha Usafiri
wa mikoa ya kusini na kuleta kichocheo cha ukuaji wa shughuli za
kiuchumi. (Picha na Mwanakombo Jumaa-Maelezo)
No comments:
Post a Comment