Na: Elizabeth Edward, Mwananchi.
SERIKALI leo inatoa hadharani ripoti ya Kamati iliyoundwa kupata taarifa kuhusu vurugu zilizotokea mkoani Iringa na kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi. Wakati ripoti hiyo ikitarajiwa kutolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Kamati nyingine iliyoundwa na Baraza la Habari (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tef), nayo leo inatarajiwa kuweka hadharani ripoti yake.
Kamati
hizo ziliundwa kwa nyakati tofauti baada ya vurugu zilizotokea Septemba
2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi wakati polisi
walipowatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakifungua tawi la chama
hicho katika kijiji hicho.
Juzi,
Makamu Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Dk Nchimbi, Theophil Makunga
alimkabidhi waziri huyo na kusema Kamati yake ilifanya ziara Iringa na
pia mahojiano na wadau mbalimbali Dar es Salaam.Kamati ya Nchimbi
ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti Jaji Steven Ihema, Makunga na Ofisa wa
Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike, Kanali Wema Wapo wa
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) pamoja na Naibu Kamishna wa Jeshi la
Polisi, Isaya Mngullu.
Tofauti
na taarifa nyingine, ripoti ya mauaji ya Mwangosi inatarajiwa kutolewa
hadharani ili umma uweze kuisoma, kuichambua na kutoa maoni kuhusu hatua
za kuchukua ili matukio ya aina hiyo yasitokee tena.
Ripoti ya MCT
Katibu Mkuu wa Tef, Neville Meena alisema timu ya uchunguzi imeshamaliza
kazi yake na leo itatoa rasmi ripoti kuhusiana na mazingira ya kifo cha
Mwangosi.
Kamati
hiyo iliundwa na watu watatu, John Mirenyi kutoka MCT, Hawra Shamte
kutoka Tef na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Saimon Berege.
“Sisi tukiwa wanahabari tuliunda Kamati yetu ili ifanye uchunguzi
kuhusiana na mauaji ya mwanahabari mwenzetu, baada ya kukamilisha
uchunguzi huo, sasa tupo tayari kuiwasilisha ripoti yetu hadharani,”
alisema Meena.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment