Mwanaharakati
mashuhuri dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Askofu Desmond
Tutu, amekabidhiwa tuzo maalum yenye thamani ya dola za kimarekani
milioni moja kutoka taasisi moja inayopigania utawala bora barani
Afrika.
Wakati ikikabidhi zawadi hiyo taasisi hiyo ya Mo
Ibrahim Foundation imemuelezea Askofu Tutu kama mmoja wa sauti muhimu
kupigania uhuru barani Afrika.
Imesema bwana Tutu aliyewahi pia kupewa tuzo ya amani ametumia maisha yake yote kupigania haki na demokrasia.
Wakfu huo wenye makao yake mjini
London,unasifika kwa kuwatuza wanaharakati mashuhuri na kutoa tuzo ya
dola milioni tano kila mwaka kwa rais mmoja wa zamani ambaye alisifika
kwa uongozi wake bora.
Tuzo hiyo imetolewa mara tatu katika miaka yake saba tangu kuzinduliwa.
No comments:
Post a Comment