Dereva kwenye ajali ya Mandela aachiliwa
Dereva wa gari
iliyohusika na ajali iliyomuua kitukuu wa rais mustaafu wa Afrika Kusini
Nelson Mandela, ameachiliwa baada ya kesi yake kutupiliwa mbali na
mahakama
Wakili wa Sizwe Mankazana, alisema kuwa mteja wake alifutiliwa madai yote dhidi yake ikiwemo kuendesha gari akiwa mlevi.
Alikuwa anamrejesha nyumbani Zenani Mandela
kutoka kwenye tamasha la kabla ya kuanza kwa kombe la dunia mwaka 2010
wakati gari lililokuwa limewabeba lilipogonga chuma.
Zenani alikuwa mmoja wa vitukuu tisa wa bwana Mandela.
Mandela aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi na
ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusin, alipigia debe
sana nchi hiyo kuandaa michuano ya kombe la dunia.
Wakili wa Mankazana,Hulme Scholes, alisema kuwa mahakimu waliitaja ajali hiyo kama ya kutisha.
Bwana Mankazana alikuwa emefutiliwa mbali makosa
yake ya kuendesha ovyo gari pamoja na kuwa mlevi, hali ambayo
ilihatarisha maisha yake.
Nyanyake Zenani sasa anasimamia kampeini ya Umoja wa Mataifa ya kuhamasisha kuhusu usalama barabarani.
Afrika Kusini ina mojawapo ya rekodi mbaya sana
za usalama wa barabarabni, na inakadiriwa kuwa watu 42 hufariki kila
siku katika barabara za nchini humo.
No comments:
Post a Comment