Mwanamke wa kwanza waziri wa Somalia
Fauzia Yusuf Haji Adan
Somalia inatarajiwa kupata
waziri wake wa kwanza mwanamke pinde baraza la mawaziri lililopendekezwa
na waziri mkuu Abdi Farah Shirdon litakapoidhinishwa na bunge.
Fauzia Yusuf Haji Adan ni mmoja wa wanasiasa
kumi waliteuliwa katika baraza la mawaziri ambalo ni ndogo sana na
ameteuliwa kama waziri wa mambo ya nje.
Alitaja kuteuliwa kwake kama jambo
la kihistoria kwa nchi hiyo na kwa wanawake wa Somalia. Bi Fauzia pia ni
naibu waziri mkuu wa Somalia.
Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa bwana Shirdon
huenda akakabiliwa na kibarua kutafuta kupitishwa kwa baraza hilo na
kuna hofu kuwa koo zote huenda zisiwakilishwe kikamilifu.
Bwana Shirdon, ambaye ni mfanyabiashara
alichukua wadhifa wake baada ya kuteuliwa na Rais Hassan Sheikh Mohamud
na hata kukubaliwa na bunge.
Uchaguzi wa bwana Mohamud mwezi Sepetemba alionekana kuwa Rais wa kwanza wa Somalia kuchaguliwa kidemokrasa kwa miaka 42.
Mawaziri hao wanachukua uongzi wa nchi ambayo
haijakuwa na uongozi thabiti kwa zaidi ya miaka 20 huku wababe wa kivita
kutoka koo mbali mbali, wapiganaji wa kiisilamu na nchi jirani za
Somalia wote wakipigania udbibiti wa Somalia baada ya kupindulia kwa
aliyekuwa rais Siad Barre mwaka 1991.
Changamoto kubwa
"Baada ya majidiliano ya muda mrefu na
kushauriana , nimeteua baraza la mawaziri, ambalo linajumuisha mawaziri
kumi. Miongoni mwao ni waziri wa kwanza mwanamke kwa mara ya kwanza
katika historia ya Somalia’’ alisema waziri mkuu.
Bi Adan anatoka katika jimbo la Somaliland lililojitenga na ameishi nchini uingereza kwa miaka mingi.
"Uteuzi wangu kama waziri wa mambo ya nje ni
jambo la kihistoria kwa Somalia na hasa kwa wanawake , inafungua ukurasa
mpya wa siasa za nchini humo na tutafanikiwa katika uongzi wetu.’’
Alisema bi Adan
Changamoto kubwa inayokabili serikali mpya inayoungwa mkono na Umoja wa matifa, ni wapiganaji wa Al shabaab.
Licha ya kupoteza baadhi ya miji mikuu,
wanamgambo hao wangali wanadhibiti sehemu kubwa za kusini mwa Somali
pamoja na maeneo ya kati.
Al-Shabab wamefanya mashambulizi kadhaa ya
kujitoa mhanga mjini Mogadishu tangu kufurushwa kwao kutoka Mogadishu na
majeshi ya Muungano wa Afrika mwaka jana ikiwemo mashambulizi kadhaa
baada ya uchaguzi wa Rais Mohamud.
No comments:
Post a Comment