Uporaji mkubwa wa Almasi Zimbabwe
Mgodi wa Marange
Almasi zenye
thamani ya dola bilioni 1.25 zimeibwa nchini Zimbabwe. Kulingana na
shirika la Partnership Africa Canada (PAC)
Shirika hilo linasema kuwa huu ndio wizi wa hali
ya juu wa Almasi kuwahi kufanywa tangu enzi ya Muingereza Cecil Rhodes
aliyekuwa mfanyabiashara mashuhuri wa Almasi.
Shirika hilo linadai kuwa wizi huo
uliofanywa katika mgodi wa Almasi wa Marange, uliwanufaisha maafisa wa
Zimbabwe, wafanyakazi wa kimataifa wa madini na makundi ya wahalifu.
Afisaa mmoja katika sekta ya madini nchini humo, alipuuza madai hayo akasema kuwa ni uongo mtupu.
Ripoti ya shirika hilo ijulikanayo kama, "Reap
What You Sow'' ufisadi na uporaji katika mgodi wa Marange, ilitolewa na
shirika hilo la nchini Canada, ikinuiwa kwenda sambamba na mkutano wa
serikali kuhusu biashara ya Almasi.
Ukiukwaji mkubwa wa sheria.
Rais Robert Mugabe, katika hotuba yake kwa
wajumbe alisema kuwa serikali itazingatia sana sheria za kimataifa
kuhusu uchimbaji wa Almasi , uhifadhi na uuzaji wake.
Almasi huishia kutengeza pete kama hizi ingawa wanaochimba wanaishi kwa umaskini mkubwa
Shirika la kimataifa la kuchunguza biashara ya
Almasi, (Kimberley Process,) iliondoa marufuku dhidi ya biashara hiyo
iliyokuwa imewekewa Zimbabwe mwaka 2011 baada ya kuungwa mkono na
Marekani pamoja na Muungano wa Ulaya.
Marufuku hiyo iliwekwa mwaka 2009, kufuatia
mauaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu katika mgodi wa Almasi
wa Marange pamoja na ripoti kuwa maafisa wa kijeshi walikuwa
wanajinufaisha na biashara haramu
Shirika la PAC lilisema kuwa ukiukwaji huo ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kutisha.
''Tunakadiria kuwa almasi za thamani ya dola bilioni mbili ziliibwa tangu mwaka 2008'' shirika hilo liliongeza.
Mwezi Julai waziri wa fedha wa Zimbabwe Tendai
Biti alisema kuwa nchi hiyo inatarajiwa kupata dola milioni miasita kama
mapato ya kigeni kutokana na mauzo ya Almasi nje ya nchi lakini
waliweza kupata tu milioni arobaini na sita.
No comments:
Post a Comment