Wanaswa baada ya jengo kuporomoka Ghana


Jengo lililoporomoka mjini Accra

Jumba la ghorofa limeporoma nchini Ghana huku watu wengi wakiarifiwa kukwama kwenye vifusi.

Waokozi wanaendelea na shughuli ya kutafuta manusura ingawa taarifa zinasema kuwa watu wawili wamefariki katika tukio hilo.

Mwandishi wa BBC Sammy Darko ambaye yuko katika eneo la tukio, anasema kuwa watu watano wameokolewa kutoka kwenye vifusi

Rais wa nchi hiyo, John Dramani Mahama, ameakhirisha kampeini zake za uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao kushughulika mkasa huo.

Naibu wake Paa Kwesi Amissah-Arthur, anaratibu juhudi za uokozi kufuatia kuporomoka kwa jengo hilo mjini Achimota .

Maafisa wanasema kuwa wanaamini takriban watu hamsini walikuwa ndani ya jengo hilo wakati lilipoporomoka asubuhi ya leo.

Mamia ya waokoaji wanawatafuta manusura kwenye vifusi kukiwa na hofu ya watu wengi kanaswa.

''Nilikuwa karibu sana na jengo hilo kwa sababu nilkuwa naenda kununua kitu madukani lakini punde nikaona jengo hilo likianza kuanguka.'' alisema makaazi mmoja Ama Okyere

"Nililazimika kukimbilia usalama wangu. Ninaamini kuwa kuna watu wengi waliokwama ndani ya vifusi kwa sababu hii ni mojawapo ya maduka ambayo yanapendwa sana na watu.'' alisema Ama Okyere

No comments:

Post a Comment