Bi Clinton alitarajiwa kuhojiwa mwaka jana lakini akaugua
Waziri wa mambo ya nje wa
Marekani, Hillary Clinton, anatarajiwa kufika mbele ya bunge la Congress
kujieleza kuhusu mashambulizi mabaya yaliyofanywa dhidi ya ubalozi wa
Marekani mjini Benghazi, Libya, mwaka jana.
Bi Clinton atakabiliwa na maswali kutoka kwa
kamati za bunge la Senate na la waakilishi kuhusu maswala ya kigeni, juu
ya usalama mbovu uliosababisha mashambulizi hayo.
Alitarajiwa kujieleza mbele ya kamati hiyo mwaka jana lakini akaugua.
Balozi wa Marekani nchini Libya Christopher
Stevens pamoja na maafisa wengine watatu wa ubalozi huo, waliuawa kwenye
mashambulizi hayo.
Balozi huyo alifariki kutokana na moshi wakati aliponaswa ndani ya jengo lililokuwa linateketea.
Hii ni baada ya wapiganaji wa kiisilamu kuvamia ubalozi.
Mashambulizi hayo yalisababisha mvutano wa kisiasa swali likuwa nani aliyekuwa na taarifa kuhusu shambulizi hilo.
Baada ya kushambulia ubalozi wavamizi walichoma bendera ya Marekani kuonyesha kero lao
Kutokana na hilo, jopo maalum lilbuniwa kuchunguza tukio hilo.
Kwa kuwa Clinton ni mwanachama wa Democrat ambao
wanadhibiti bunge la Senate, atakuwa anahojiwa kwa njia ya heshima
lakini atakabiliwa na wakati mgumu kutoka kwa wabunge wa bunge la
waakilishi ambao wengi ni wanachama wa Republican.
Jopo hilo huenda lisimlimbikizie lawama sana
Clinton kwa utovu wa usalama kwenye ubalozi huo, lakini wanachama wa
Congress bado watataka kujua kwa nini hakuwa na taarifa kuhusu ombi la
kuimarisha usalama katika ubalozi huo.
Pia atakabiliwa na maswali kuhusu ambavyo serikali ya Obama ilishughulikia mzozo huo.
Wafanyakazi watatu wa serikali walifutwa kazi
kuhusiana na shambulizi la Benghazi na mapendekezo yaliyotolewa na jopo
hilo mwezi Disemba tayari yanashughulikiwa.
No comments:
Post a Comment