Mji wa Konza unatarajiwa kuwa mji mkubwa wa kiteknoljia barani Afrika
Kenya imechukua hatua ya kwanza
katika ujenzi wa kile inachotarajia utakuwa mradi mkubwa zaidi barani
Afrika wa mji wa kiteknolojia (silicon Valley) au unaotegemea sana vifaa
vya elektroniki katika kuendeleza teknolojia ya habari na mawasilaino
ili kukuza uchumi.
Rais Mwai Kibaki amezindua rasmi mradi huo
katika eneo la Konza , mtaa mdogo Kusini mwa Nairobi, ambako mji huo
mpya wa kiteknolojia utajengwa katika muda wa miaka 20 ijayo.
Mji huu unatarajiwa kuibadili sura ya Kenya kuwa kitovu cha kwanza Afrika cha teknolojia ya habari na mawasiliano.
Mradi huu wenye thamani ya dola bilioni kumi na
nne na nusu upo chini ya mpango wa wizara ya habari na mawasiliano.Iwapo
utakamilika, Mji wa kiteknolojia wa Konza utajumuisha bustani, makaazi
na mijengo ya kibiashara na kijamii.
Ujenzi wa mji wa Konza ni mradi katika ruwaza ya
maendeleo Kenya kufikia mwaka 2030 na unalenga kuimarisha maisha kwa
taifa zima na kulifanya kuwa na ushindani duniani ifikapo mwaka huo
2030.
Rais Mwai Kibaki ameeleza kuwa ujenzi wa Mji wa Konza utasaidia kubadili uchumi wa Kenya kwa ukubwa.
Mradi wa mji wa Konza unanuia kuendeleza viwanda
vya huduma za teknolojia hiyo ya mawasiliano, na mfumo wa kupata
biashara kutoka nchi za nje ili kutafuta utajiri wa mali na kutoa nafasi
za ajira.
Mradi huu unasemekana kutoa nafasi zaidi ya laki
moja za ajira ifikapo mwaka 2030 pamoja na kuendelea kudumisha ukuwaji
wa pato jumla la nchi la asilimia 10 katika kipindi cha miaka kumi na
nane ijayo.
Wizara ya habari na mawasiliano nchini ilipewa
jukumu la kuidhinisha mradi huo kupitia makubaliano ya baraza la
mawaziri lililouidhinisha miongoni mwa miradi mingine ili kukuza na
kuendeleza sekta hiyo ya teknolojia ya mawasilino nchini.
Suali ambalo linasalia ni kuna umuhimu gani
katika ulimwengu wa sasa ulioendelea kitenolojia kwa ujenzi wa mji huu
na watu kuuhamia mji wa Konza?
No comments:
Post a Comment