Waziri Wizara ya Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe
Wizara ya Uchukuzi imethibitisha kupokea rasmi
ripoti ya mapendekeo yaliyotolewa na Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA) dhidi ya viongozi wandamizi wa mamlaka hiyo
waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi kwa ajili ya
maamuzi ya mwisho.
Waziri wa wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, aliiambia NIPASHE jana kuwa baada ya kurejea kutoka katika ziara mkoani Tabora aliikuta ripoti hiyo ofisini kwake.
Alhamisi iliyopita gazeti hili lilichapisha habari ikisema kuwa ripoti ya uchunguzi dhidi ya maofisa hao imewasilishwa katika ofisi ya Waziri Mwakyembe, lakini waziri huyo alisema asingeweza kuthibitisha kwa kuwa alikuwa katika ziara ya Rais Jakaya Kikwete mkoani Tabora.
Dk. Mwakyembe hata hivyo, hakuweka wazi ni lini maamuzi ya kuwachukulia ama kutowachukulia hatua viongozi hao yatafanyika.
Wiki iliyopita gazeti hili lilidokezwa kuwa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari imemaliza kuwahoji viongozi hao wandamizi na kuwasilisha mapendekezo kwa Waziri kwa maamuzi ya mwisho.
Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria za Bandari, maamuzi kuhusu hatma ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ephraem Mgawe, ambaye ni miongoni mwa vigogo sita waliosimamishwa kazi, hayaihusu Bodi bali Waziri.
Taarifa zilieleza kuwa bodi imemaliza kumhoji Mgawe na kupoke
a utetezi wake na kwamba taarifa ya uchunguzi dhidi yake iliwasilishwa mezani kwa Waziri Mwakyembe tangu wiki iliyopita.
Agosti mwaka jana, Dk. Mwakyembe alimsimamisha kazi Mgawe, na maofisa wengine waandamizi sita kufuatia tuhuma za ufisadi katika mamlaka hiyo.
Wengine waliosimamishwa ni manaibu wakurugenzi wawili wa TPA, Julius Mfuko (Maendeleo ya Miundombinu); Hamad Kashuma (Huduma); Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ng’amilo na mameneja wawili wa Bohari ya Mafuta Kurasini Oil Jetty (KOJ) pamoja na mhandisi wa bohari hiyo.
Hatua ya bodi kuwahoji vigogo hao inafuatia kukamilika kwa taarifa ya uchunguzi dhidi ya menejimenti ya TPA. Waziri Mwakyembe ndiye aliyeagiza uchunguzi dhidi yao ufanyike Agosti mwaka jana.
Agosti mwaka jana, Mwakyembe alipozungumza na waandishi wa habari, alisema kuwa vigogo hao wamesimamishwa kwa muda ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazoikabili menejimenti ya TPA zikiwamo wizi wa makontena, wizi wa mafuta, udokozi wa mizigo na rushwa katika utoaji wa huduma.
Alisema kumekuwa na wizi usioisha bandarini kiasi cha kutishia uhai wake kwa kuwa unafukuza wateja ambao wamehamia bandari za Mombasa nchini Kenya na Durban, Afrika Kusini ambako hakuna kero hizo.

No comments:
Post a Comment