Watu 60 wafariki kwenye sherehe za mwaka mpya Ivory Coast
Mavazi ya watu nwaliouawa kwenye msongamano mjini Abidjan
Zaidi ya watu sitini wamefariki
na wengine mia mbili kujeruhiwa katika pwani ya Ivory coast katika
sherehe za kuukaribisha mwaka mpya.
Kisa hicho kilitokea kufuatia msongamano wa watu wakati wa sherehe hizo, za kuukaribishwa mwaka mpya wa 2013.
Vyombo vya habari vya taifa hilo vinasema tukio hilo lilitokea mapema alfajiri katika jiji kuu la Abijdan.
Inasemekana kuwa watu hao walikuwa wakishuhudia maonyesho ya fataki katika uwanja wa michezo.
Wengi waliofariki ni watoto kati ya miaka minane hadi kumi na mitano.
Hata hivyo haijulikani kilichosababisha msongamano huo.
Ajali hiyo ilitokea katia uwanja wa michezo wa
Felix Houphouet Boign, ambao una ukumbwa wa kuruhusu mashabiuki elfu
sitini na tano wa soka na ulipewa jina hilo kama heshima ya rais wa
kwanza wa nchi hiyo.
Kabla ya ajali hiyo uwanja huo uliandaa maonyesho ya muziki iliyohudhuriwa na mwana muziki kutoka Marekani Chris Brown.
No comments:
Post a Comment