WATAKIWA KUTUNZA MIUNDOMBINU
Na John
Banda, Dodoma
Wakazi wa
kitongoji cha Msangalalee kata ya Dodoma Makulu Manispaa ya Dodoma wametakiwa
kuilinda na kuitunza miundombinu ya maji safi iliyopo kwenye maeneo yao ili
iweze kudumu kwa muda mrefu.
Kauli hiyo
ilitolewa jana na mwenyekiti wa kitongoji hicho William Chacha wakati
akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kitongoji hicho.
Chacha
alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu ambao huwa
wanaharibu miundombinu ya maji kwa makusudi na kusababisha adha ya maji katika
eneo hilo.
Alimtaka
kila mtu kuwa mlinzi wa miundombinu ya hiyo ili huduma hiyo muhimu iwe endelevu
kwa kupatikana kila wakati kwaa jili ya manufaa ya kila mmoja.
“Nimepata
taarifa kuwa kuna watu wanang’oa mabomba ya maji na kwenda kuyauza kama vyuma
chakavu, hilo ni kosa kisheria na kama tukikubaini tutakufikisha mahakamani kwa
kosa la uharibifu wa miundombinu ya maji ambapo adhabu yake utaijua hukohuko
mbele,” alisema Chacha.
Aliongeza,
ni jukumu la kila mwananchi kulinda mabomba hayo ya maji safi kwani ndiyo chanzo
pekee cha majisafi katika kitongoji hicho ambacho kimeanza kupata huduma ya
majisafi mwaka huu tangu uhuru.
Akizungumza
katika mkutano huo, mmoja wa wakazi wa kitongoji hicho Lesca Chedego
aliipongeza mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mjini hapa (DUWASA) kwa
kuwafikishia huduma hiyo muhimu ya maji wakazi wa kitongoji hicho.
Kitongoji
cha Msangalalee kimeanza kupata huduma ya majisafi tangu mwezi wa sita mwaka
huu ambapo gharama za mradi huo ziligharamiwa na Duwasa kwa kuweka vituo (Domestic
Points (DP)) 6 katika kitongoji hicho.
Mwisho
No comments:
Post a Comment