AU yazidisha vita dhidi ya Al Shabaab
Al Shabaab
Mamia ya wanajeshi wa Muungano wa Afrika
wanaukaribia mji muhimu wa Koryoley, ulio umbali wa kilomita 90 Kusini
Magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.
Mji wa Koryoley, umekuwa chini ya udhibiti wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab kwa miaka mitano iliyopita.
Mwandishi wa BBC aliye katika eneo hilo anasema kuwa wanajeshi hao wako umbali wa kilomita 10 kutoka mjini humo.
Anasema kuwa ikiwa wanajeshi hao wataukomba mji
huo, utakuwa ukombozi wao mkubwa wa mji tangu kuanza harakati hizo dhidi
ya Al Shabaab mwezi Machi mwaka jana wakiungwa mkono na Umoja wa
Mataifa.
Wanajeshi hao wamefanikiwa kukomboa miji mingine muhimu na hata kuwatimua wapiganaji hao kutoka katika ngome zao kubwa.
Wengi wa wanajeshi wa AU ni kutoka Uganda,
wakisaidiwa na wanajeshi wa Kenya, Burundi na sasa Ethiopia pamoja na
wanajeshi wa Somalia.
No comments:
Post a Comment