Shirika la haki za binadamu
Human Rights Watch linasema makumi kadhaa ya watu waliuawa katika ghasia
zinazoendelea katika jimbo la Darfur nchini Sudan.
Shirika hilo linasema viongozi wa kijamii katika
vijiji viwili wametoa orodha ya majina ya raia takriban arobaini
waliouawa katika wiki chache zilizopita kwenye makabiliano baina ya
vikosi vinavyounga mkono serikali na vile vya waasi.
Human Rights Watch linasema wanavijiji wengine
makumi kadhaa walishambuliwa, baadhi yao wakipigwa na makombora ya ndege
za kijeshi. Shirika la msalaba mwekundu limesema mmoja wa wafanyakazi
wake aliuawa jana.
Umoja wa Mataifa unasema mwaka huu pekee zaidi ya watu laki mbili wameyakimbia makazi yao jimboni Darfur.
No comments:
Post a Comment