Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanya, Benson Mpesya akitoa maelekezo kwa fundi ili kufungua mlango unaodaiwa kufungwa na diwani na watu wengine watatu. Picha: Mohab Dominick.
Watu watatu akiwamo Diwani wa Kata ya
Mwendakulima ya Halmashauri ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga,
Ntabo Majhabi wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufunga ofisi za
serikali za mtendaji wa kata hiyo.
Wanadaiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita asubuhi baada ya mtendaji wa
kata hiyo, Cecilia Clement kupigiwa simu na mlinzi wa ofisi hizo,
Joseph Katambi na kumpa taarifa za tukio hilo liliofanywa na wananchi 15
walioambatana na diwani huyo.
Kwa mujibu mtendaji huyo, waliamua kuibadilisha kamati ya sungusungu ya
kata hiyo hali ambayo ilianza kuleta malalamiko na minong’ono na kwamba
huenda ni chanzo cha watuhumiwa hao kufunga ofisi hizo.
Aliwataja wengine walikamatwa kuwa ni fundi selemala,Hamisi Abbas na Makaka Benedictor, wakazi wa kata hiyo.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya akiongozana
na kamati ya ulinzi ya kata na askari polisi, walifika katika ofisi
hiyo kushuhudia mlango huo ulivyofungwa kwa kuwekewa kipande cha bati
na kupigiliwa misumari na mawe.
Mpesya alitoa amri ya kuvunjwa kwa bati hilo chini ya ulinzi wa polisi
na kuamuru waliohusika akiwamo diwani huyo kukamatwa na kutiwa mbaroni.
Akizungumzia kitendo hicho Mpesya, alisema ni fedheha na kisichoweza kuvumilika .
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment